Messi anaamini yeye ni mchezaji huru, Barcelona yadai bado ana mwaka mmoja, Je tukio hili linafanana na la Morrison ?

Mshambuliaji hatari duniani, Lionel Messi ambaye ameingia katika gumzo mitandaoni na vyombo vya habari vya Kimataifa juu ya hatma yake ndani ya Barcelona baada ya kuomba kwa uongozi wa klabu hiyo kutaka kuondoka.

Lionel Messi transfer: Only Manchester City or PSG could afford ...

Messi kwa upande wake anaamini sasa ni Mchezaji huru na anaweza kwenda kujiunga na klabu yoyote. Hilo ni tofauti na Barcelona ambao kwa upande wao wanadai bado ana mwaka mmoja na akiwa na ‘release clause’ ya paundi milioni 629.

Kama Manchester City itaamini maneno ya Messi ni sahihi kuwa yupo huru italazimika kupata ‘provisional international transfer certificate (ITC) kutoka Shirikisho la soka duniani FIFA na kumsajili ili kuanza kuwatumikia msimu huu mpya unaokuja.

Mpaka sasa FIFA ndiyo yenye uwezo wa kuamua mzozo utakaojitokeza kati ya Barcelona na Manchester City inayotaka kumsajili Messi kwaajili ya msimu ujao.

Lionel Messi hands in Barcelona transfer request: Where could he ...

Kama FIFA itasema Messi yupo sahihi kuwa ni mchezaji huru basi moja kwa moja atajiunga na Man City. Lakini kama FIFA iasema Barcelona ndiyo ipo sahihi basi City italazimika kutoa ‘release clause’ kama inamuhitaji.

Mkataba wa mwisho Messi aliyoanguka saini mwaka 2017 ulimpa ruksa ya kuondoka bure kila ifikapo mwisho wa msimu kama atahitaji kufanya hivyo na kutoa taarifa mapema katika siku 10 za kwanza za mwezi Juni.

Na kama endapo hakutakuwa na taarifa zozote kutoka kwa Messi za kuomba kuondoka baada ya kupita siku 10 za mwanzo za mwezi Juni, klabu itachukulia kuwa dirisha hilo limepita kwa maana hiyo atakuwa kwa mwaka mwengine ndani ya timu.

Lakini Messi yeye anatafsiri tofauti, kama mkataba unamruhusu kuondoka kama mchezaji huru kila mwisho wa msimu na msimu huu haukuisha hadi mwezi Agosti, hivyo anaamini anaweza kwenda pasipo malipo.

Lionel Messi - Player profile 20/21 | Transfermarkt

Nchini Tanzania kulikuwa na sakata la usajili la mchezaji Bernard Morrison, ambapo Uongozi wa klabu ya Yanga ulisema kuwa ni mchezaji wao halali kwakuwa alikuwa na mkataba wa miaka miwili. Wakati huo huo nyota huyo ambaye alishamwaga wino Simba SC akidai kuwa alikuwa ni mchezaji huru na mkataba wake ulishamalizika.

Utata huo ambao mwisho wa siku uliamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji na kutoka na majibu kuwa Morrison alikuwa ni mchezaji huru.

SimbaDay: Bernard Morrison Kicks Off Simba SC Career On A Flier (+ ...

Je katika sakata hili la Messi, Barcelona na kwa mbali likihusisha na Manchester City litakuja na majibu gani ?

NILIYEANDIKA JINA LANGU HAMZA FUMO, INSTAGRAM @fumo255

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW