Burudani ya Michezo Live

Messi ashinda tuzo ya BallonDor2019, Afrika yatoa watatu kumi bora BALLON D’OR 2019

Nahodha wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, ameshinda tuzo ya BallonDor2019 katika sherehe zilizofanyika usiku huu Jijini Paris Ufaransa.

Messi amewashinda beki wa Liverpool Virgil van Dijk aliyeshika nafasi ya pili, pamoja na Cristiano aliyekamata nafasi ya tatu huku Sadio Mane akiwa nafasi ya nne.

Aliyeshika nafasi ya tano ni mshambuliaji wa Liverpool , Mo Salah, nafasi ya sita imekwenda kwa mshambuliaji wa PSG na Ufaransa, Kylian Mbappe, nafasi ya saba ikarudi Liverpool kwa golikipa Mbrazil Allison Becker ambaye pia ndiye mshindi wa tuzo ya golikipa bora.

Namba nane ni straika wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowsk, namba tisa ni Bernardo Silva wa Man City na namba 10 ni Mwafrika Riyard Mahrez kutoka Algeria akikiwasha pale Man City nchini England.

Hili ni taji lake la 6 na hivyo amemzidi Cristiano Ronaldo mwenye mataji 5 mpaka sasa.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW