Michezo

Messi athibitisha ubora wake mbele ya Eibar

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC Barcelona, Lionel Andres “Leo” Messi ameendelea kuonyesha ubora wake katika ligi kuu nchini Hispania, La Liga baada ya kufunga magoli manne katika mchezo dhidi ya Eibar wakati wakichomoza na ushindi wa jumla ya mabao 6-1.

Messi mwenye umri wa miaka 30, ameiongoza timu yake kuchomoza na ushindi wa mabao hayo baada ya kuanza kuifungia kwa njia ya mkwaju wa penati dakika 20, kisha kufunga tena dakika ya 59, kisha kutupia tena 62 na kumalizia bao lake la nne  87, huku mchezaji, Palinho akifunga bao moja na Denis Suarez akifunga moja.

Katika mchezo huo Lionel Messi amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo ‘Man of the Match’ huku baadhi ya watu wakiamini kuwa muargentina huyo kaishiwa kiwango licha ya yeye kuthibitisha ubora aliyonao katika soka .

Kwa kuisaidia Barca kuchomoza na ushindi huo sasa timu hiyo inaongoza katika msimamo wa La Liga kwa kuwa na pointi 15 huku Sevilla ikiwakaribia kwa ukaribu kwakuwa na alama 10 huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na Valencia kwakuwa na alama 9.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents