Burudani ya Michezo Live

Messi kujiunga na Cristiano Ronaldo ndani ya Juventus ?, picha kamili lipo hivi

Messi kujiunga na Cristiano Ronaldo ndani ya Juventus ?, picha kamili lipo hivi

Mchezaji bora kabisa kunako mchezo wa soka duniani, Lionel Messi amevunja mazungumzo ya kuongeza kandarasi yake na viongozi wa Barcelona hali iliyotafsriwa kuwa anahitaji kuondoka LaLiga.

Kitendo cha Messi kuvunja mazungumzo hayo wachambuzi wa mbambo wanadai kuwa muda umefika sasa wa nyota huyo wa Argentina kuondoka na kwenda kuandika historia sehemu nyingine.

Mwaka 2001, Lionel Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 14. Kwenye jumla ya michezo aliyocheza 480 amefunga jumla ya magoli 441 na sasa kufikisha mabao 700 ukijumuisha na ndani ya timu yake ya taifa. Hakuna ubishi Messi ndiyo mchezaji bora zaidi ulimwenguni kwa sasa .

Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2021, wakati mara ya mwisho kusaini ilikuwa mwaka 2017, pengine ipo sababu ya nyota huyo kukataa mazungumzo ya kuongeza mkataba na waajiri wake.

Mshindi huyo mara sita wa tuzo za Ballon d’Or inadaiwa kuwa huwenda akajiunga na moja ya timu za Italia ambapo kuna mpinzani wake Cristiano Ronaldo.

Mbali na Manchester City kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Lionel Messi lakini pia Juventus inahitaji kumsajili mchezaji huyo na hivyo kuzua gumzo kuwa itawezekana vipi mafahari wawili kukaa zizi moja.

Itawezekana vipi Messi kucheza pamoja na  Cristiano Ronaldo katika timu moja, ikiwa hilo halijawahi hata kutokea kwenye timu zinazo undwaa kwaajili ya kucheza mechi za kutoa msaada kwa watu wasiojiweza.

Mwaka 2018, Ronaldo aliwahi kumshauri Messi ajiunge na yeye na kudai kuwa lazima atakuwa amemmisi “Pengine Messi amenimisi”.

“Nimecheza England, Hispania, Italy, Ureno na katika timu yangu ya taifa wakati yeye bado amesalia pale pale Hispania.”

“Pengine ananihitaji mimi zaidi,  kwa upande wangu maisha ni changamoto, napenda kukutana na changamoto mpya na napenda kuwafanya watu wawe na furaha.”

“Napendelea yeye aje Italy siku moja. Natumaini atakubali changamoto kama mimi, lakini kama ni mwenyefuraha sehemu alipo basi naheshimu hilo.”

“Yeye ni mchezaji bora na mtu mzuri, lakini mimi sina ninachokimisi hapa. Haya ni maisha yangu mapya na najisikia ni mwenye furaha.”

Imeandikwa na Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW