Michezo

Messi kukaa nje kwa miezi miwili

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili ijayo kufuatia jeraha la goti.

az1

Mshambuaji huyo wa Argentina aliumia katika mechi ya ligi kuu ya Hispania dhidi ya Las Palmas ambapo Barcelona ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2-1.

Messi, 28 aliondolewa uwanjani na kukimbizwa hospitali katika dakika ya 3 ya mechi hiyo. Kocha Luis Enrique alisema atajitahidi kuendeleza mfumo wa mchezo wao hata bila ya Messi kuwepo.

“Kutokuwepo kwa Messi ni pigo ila tutalazimika kujifunga kibwebwe, na hili ninamaanisha kila mchezaji wetu atajikaza kisabuni ili kuziba pengo hilo japo ni kubwa,” alisema.

mun1
Kocha wa Barcelona, Luis Enrique (kulia), akimfariji Messi, baada ya kupata majeraha

“Unajua ni vyema kuwa Messi si mchezaji wa kawaida, mara nyingi amezinyima usingizi safu za ulinzi za timu nyingi wakati ambao hata mimi mwenyewe nahisi nimejitolea mzima mzima,” aliongeza Enrique.

Huenda mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora duniani akarejea katika mechi baina ya Barcelona na wapinzani wao wa jadi Real Madrid Novemba 22.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents