Michezo

Messi ndiyo ‘mbabe’ wa Ulaya msimu huu (+Video)

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona, Lionel Messi ndiyo mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi kwenye ligi kubwa tano Barani Ulaya kwa msimu huu kwa kutupia magoli 37 ya Ligi.

Tokeo la picha la messi
Lionel Messi

Messi ambaye mapema mwa mwezi uliopita alikataa kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Barcelona, ametupia magoli 37 kwenye Ligi ya Uhispania (Laliga) akiwa amewazidi wachezaji wenzake wote wanaokipiga kwenye Ligi kubwa tano Barani Ulaya ambao ni Edinson Cavani mwenye magoli 35 kutoka PSG ya Ufaransa,Pierre-Emerick Aubameyang Magoli 30 kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani,Harry Kane magoli 29 kutoka Spurs ya Uingereza na Edin Dzeko magoli 28 kutoka Klabu ya Juventus ya Italia .

Messi sasa atachukua kiatu cha mfungaji bora kwa msimu huu barani ulaya kwa mara ya nne na kwa rekodi hiyo atakuwa amemfikia mshambuliaji wa real madrid, Cristiano Ronaldo ambae na yeye amechukua kiatu hicho mara nne.

Tazama hapa chini magoli mawili ya Messi ya jana usiku dhidi ya Eibar.

https://youtu.be/ra63dDY2yjk

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents