Michezo

Messi Vs Ronaldo; Mourinho avunja ukimya amuweka hadharani mchezaji wake bora wa muda wote

Kocha mwenye mafanikio makubwa kunako soka, Jose Mourinho ‘The Special One’ ameamua kumuweka hadharani yupi ni mchezaji wake bora ambaye anaona kwa pande wake anamuona nastahili kuchukua nafasi hiyo.

Image result for jose mourinho

Mourinho mwenye historia kubwa katika kabumbu hasa kutokana na kupata bahati ya kuwafundisha nyota wengi wakubwa ameamua kufunguka ya moyoni kwa upande wake ili kuepuka kuulizwa swali lile lile nani ni mchezaji wake bora.

Kocha huyo wazamani wa Manchester United amewahi pia kuwafundisha, Didier Drogba, Zlatan Ibrahimovic, Samuel Eto’o na wengine wengi na hivyo kujijengea jina na heshima kubwa kwenye soka.

Alipoulizwa kwa upande wake anadhani yupi ni mchezaji bora Messi na Ronaldo, Mreno huyo alimtaja ‘legend’ wa Brazil, Ronaldo De Lima.

Mourinho ambaye amewahi kumfundisha Ronaldo De Lima ndani ya Barcelona akiwa kama kocha msaidizi chini ya meneja mkuu, Bryan Robson anaona yeye ndiyo mchezaji bora kwa upande wake.

Mourinho, Robson and Ronaldo finished second in La Liga but won the 1997 Cup Winners' Cup

Mreno huyo mwenye umri wa miaka 56 anaamini hakuna mchezaji kwenye historia ya soka anayeweza kuzidi kipaji alichokuwa nacho Ronaldo ambaye kwa sasa ameshakuwa mtu mzima na umri wa miaka 43.

‘’Nilipokuwa Barcelona na Bobby Robson, ndipo nipogundua Ronaldo ni mchezaji bora kabisa kuwa kumuona uwanjani,” Mourinho alipoiyambia Live Score huku akisema kuwa goli lake la mwaka 1997 kati ya Barca dhidi ya PSG lililofahamika kama  he remains confounded by a goal the Brazilian scored for Barca against PSG in Rotterdam in 1997, calling ‘awesome’ bado limebaki akilini.

Jose Mourinho ameongeza ‘‘Majera ndiyo yaliuwa kipaje chake na kushindwa kufanya maajabu makubwa zaidi, lakini kipaji chake kwa wakati huo akiwa na umri wa miaka 19 ulikuwa unaona kuwa anauwezo wa hali ya juu.”

‘’Cristiano Ronaldo na Leo Messi wao kwa upande wao wamekuwa na muda mrefu kwenye soka ndiyo maana wameweza kuonyesha uwezo wao, wamekuwa kwa zaidi ya miaka 15. Hata hivyo ukizungumzia uwezo, kipaji basi hakuna atakayepingana na mimi kuhusu Ronaldo.’’

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents