Messi vs Ronaldo; Nani atakaye maliza maisha ya soka akiwa na magoli mengi zaidi ya mwenzie?
Kwa upande mwingine watu wanamtazamia, Messi kama ananafasi kubwa zaidi ya hasimu wake Ronaldo kutokana na kuwa na umri mdogo wa miaka 32 dhidi ya 35 aliyokuwa nayo Mreno licha ya nyota huyo wa Juventus kukusudia kulitumikia soka mpaka atakapo fikisha miaka 40 ndipo atakapotundika daluga.
Mara kadhaa, Messi amekuwa akisumbuliwa na majeraha na hivyo kusababisha kupunguza spidi yake ya upachikaji mabao lakini bado amekuwa akiendelea rekodi zake mwenyewe.
Akicheza michezo 31 ndani ya klabu ya Sporting CP, na kufunga mabao matano 5, magoli 118 katika mechi 292 Manchester United, Ronaldo aliendeleza moto wake huko Hispania baada ya kuifungia Real Madrid magoli 451 kwenye michezo 438 aliyoshuka uwanjani na kwa sasa kiumbe huyo anafanya yake pale Turin, ashafunga mabao 32 katika mechi 51.
Kwa tafsri nyepesi tu, kiumbe huyu ana asilimia 47 ya kufunga bao kila dakika 112 kwenye michezo aliyocheza na kwa sasa anakimbizia rekodi ya mchawi wa soka Muaustralia, Josef Biscan aliyefunga magoli 805.
By Hamza Fumo