Burudani

Mesut Ozil aagana na ukapela, Rais wa Uturuki, Erdogan awa mshenga wa harusi hiyo

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekuwa mshenga katika ndoa ya wa mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil hapo jana siku ya Ijumaa mjini Instabul nchini Uturuki.

Erdogan attended the wedding of Ozil, who is of Turkish descent [Murat Cetinmuhurdar/Reuters]

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani, Ozil alitangaza mwezi Machi mwaka huu alisema kwamba alimuomba rais Erdogan kuwa mshenga wake swala ambalo lilizua hisia kali nchini Ujerumani.

Helge Braun, waziri wa Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliambia gazeti la Bild kwamba ilikuwa uchungu sana kumuona Ozil akimchagua kiongozi kama huyo baada ya shutuma alizopata na rais huyo wa Uturuki mwaka uliopita.

Erdogan na Ozil

Rais Erdogan na mkewe Emine (kulia) wakipiga picha na wanandoa hao

Ozil ambaye chimbuko lake ni Uturuki, alishangaza watu wengi pale alipopiga picha na rais wa nchi hiyo Erdogan kabla ya kombe la dunia mwaka uliopita.

Kasha kutangaza kustaafu Kimataifa kuitumikia timu yake ya taifa ya Ujerumani kutokana na madai ya ubaguzi wa rangi na kutoheshimiwa baada ya picha hizo kusambaa nchini Ujerumani.

Kiungo huyo wa Arsenal alimuoa mpenzi wake malkia wa urembo wa Uturuki, Amine Gulse katika hoteli moja ya kifahari karibu na kingo za mto Bosphorus.

Wanandoa hao walianza kuchumbiana 2017 na kutangaza kilichokuwa kikiendelea kati yao mwezi Juni mwaka 2018.

Ozil na Gulse ambaye amekuwa Uturuki mwaka 2014, wamekusanya mchango kwa Turkish Red Crescent ili kuwapatia chakula zaidi ya wakimbizi 15,000 kutoka Syria.

Bwana Erdogan wakati huohuo aliripotiwa kwamba ni nadra sana kwa yeye kuhudhuria harusi nchini Uturuki hususan wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hatua yake ya kuhudhuria harusi ya Ozil inajiri wakati ambapo uchaguzi wa marudio wa Meya unasubiriwa mjini Instanbul.

Matokeo ya awali yalionyesha kwamba mgombea wake wa chama cha APK alishindwa kwa kura chache hatua iliopelekea uchaguzi huo kufutiliwa mbali na hivyobasi kuzua hisia kali za kimataifa.

Ni nini kilichotokea mwaka uliopita?

Raia huyo wa kizazi cha tatu cha Ujerumani na Uturuki alizaliwa katika mji wa Gelsenkirchen na alikuwa kiungo muhimu wa timu yataifa ya kombe la dunia ilioshinda 2014

Ameichezea Ujerumani mara 92 na mashabiki wamempigia kura kuwa mchezaji bora wa timu ya taifa mara tano tangu 2011.

Lakini mnamo mwezi Mei Ozil alizua hisia kali nchini Ujerumani alipopiga picha na rais wa Uturuki kabla ya kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na kuwafanya wengine kujiuliza maswali kuhusu taifa analolitii.

Lakini ukosoaji huo ulizidi baada ya timu ya taifa ya Ujerumani kubanduliwa katika mashindano hayo katika raundi ya kwanza.

Sherehe ya harusi ya Ozil

Baada ya kushindwa , Ozil alichapisha taarifa ndefu akitangaza kustaafu katika timu ya taifa ya Ujerumani.

Alisema kwamba alipokea barua za chuki na kwamba alikuwa analaumiwa kwa kushindwa kwa Ujerumani nchini Urusi .

”Mimi ni Mjerumani pekee tunaposhinda lakini mimi ni mhamiaji tunaposhindwa”, alisema Ozil akiongezea kuwa licha ya historia yake ya ufanisi na timu hiyo ya taifa jinsi alivyokemewa kulimfanya kutotaka tena kuvaa jezi ya timu ya taifa ya Ujerumani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents