Burudani ya Michezo Live

Mexico: Maharamia washambulia meli

Jeshi la wana maji nchini Mexico limesema jana kuwa maharamia wameshambulia meli iliyokuwa na bendera ya Italia katika ghuba ya Kusini ya Mexico na kuwajeruhi wafanyikazi wawili wa meli hiyo katika shambulizi la hivi punde zaidi la wizi na uharamia kukumba sekta ya mafuta na miundo mbinu katika eneo hilo.

Image result for italian ship attacked mexico

Katika taarifa, jeshi hilo limesema kuwa mmoja wa wafanyikazi hao alipata majeraha ya risasi na mwengine kupata mshtuko na wote wawili kuhamishwa hadi katika hosipitali iliyokuwa karibu.

Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Micoperi nchini Italia, hutumika kwa usambazaji katika sekta ya mafuta nchini Mexico.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari katika eneo hilo, boti hilo lilikuwa na wafanyikazi 35 wakati shambulizi hilo lililopotekelezwa kando ya mji wa Ciudad del Carmen katika jimbo la Campeche.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW