Habari

Meya Sitta aahidi Kinondoni kujiendesha kwa mapato yake ya ndani

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta amesema kuwa licha ya serikali kuu kuchukua baadhi ya vyanzo vya mapato vya Halmashauri hiyo ikiwemo Kodi ya Bango, Huduma, na Majengo, halmahauri hiyo inatarajia kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ili iweze kusimamia baadhi ya miradi ya manispaa hiyo.

Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta akiendesha kikao.

Meya Sitta ameongeza kuwa pamoja na vyanzo hivyo vya mapato kuchukuliwa na serikali lakini imekuwa ikiwasaidia kulipa baadhi ya fidia ikiwemo fidia ya mradi wa DMDP ambapo serikali imeilipia Manispaa kiasi cha shilingi bilioni moja.

“Sisi kama Kinondoni tunaangalia namna ambavyo tunaweza kuongeza vyanzo vyetu vya mapato ili ifike wakati baadhi ya miradi yetu tuiendeshe wenyewe. Kama mnavyojua tayari serikali kuu imeshachukua baadhi ya vyanzo vya mapato lakini tayari tumeweka mikakati yetu thabiti kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili tuendeshe miradi yetu,” alisema Meya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli ameeleza kuwa vyanzo vya mapato vilivyochukuliwa na serikali kuu, serikali imeamua kukusanya mapato kwa niaba ya Halmashauri.

Huku Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameitaka serikali kuhakikisha inapofanya marejesho ya mapato ya vyanzo vya Halmashauri ilizo zichukua kwa kiwango kinachoridhisha ili Halmashauri iweze kuendesha miradi yake ipasavyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents