Habari

Meya Sitta afunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi kwa namna ya kipekee

Meya wa Kinindoni Benjamin Sitta  Serikali  imesema inampango mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi na kutoa ajira za uhakika kwa Watanzania ambao wanafanya shughuli hiyo.

Meya amesema hayo akiwa Msasani Soko la Samaki wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi kwa wavuvi waliofanya vizuri katika mashindano yakuvua samaki kwa vitumbwi na ngalawa yalioandaliwa na taasisi ya Tuna ambapo mshindi wa kwanza alipata tsh 400,000, wapili tsh 300,000 na wa tatu tsh 200,000.

Alisema serikali  imesema  inampango mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi ili sekta hiyo iweze kufanya vizuri na kusonga mbele zaidi

Meya alisema wavuvi  wanapaswa kuwa wabunifu ili kusaidia sekta hiyo kufanya vizuri zaidi.

Afisa Uvuvi wa Manispaa Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza katika kilele hicho

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents