Tupo Nawe

Meya Sitta aja na mfumo huu kwa sekondari ”Mwalimu mmoja atafundisha shule zote za Kinondoni kwa wakati mmoja, wanafunzi watakuwa Live” (+video)

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh.Benjamin Sitta ametangaza kufunga mifumo ya teknolojia katika shule zote za sekondari za wilaya hiyo ambayo itamuwezesha mwalimu mmoja kufundisha idadi kubwa ya wanafunzi kwa mara moja huku wakiwa na uwezo wa kuonana na hata kuulizana maswali na kujibiwa papo hapo.

Mh. Sitta amesema mwalimu mmoja bingwa atakuwa na uwezo wa kufundisha wanafunzi wa shule zote za sekondari za serikali kwa wakati mmoja huku lengo kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu ya kiwango cha juu na kusisitiza kuwa mfumo huo utakuwa ni wa kwanza hapa nchini Tanzania na hata Afrika Mashariki na Kati.

”Ni muendelezo wa programu yetu ambayo tunakaribia kuizindua, Mwalimu mmoja bingwa atakuwa na uwezo wa kufundisha shule zote za sekondari za serikali.”

Mh.Benjamin Sitta ameongeza ”Mfumo huu utakuwa wa kwanza Tanzania na hata Afrika Mashariki na Kati, lengo ni kumsaidia mtoto wa maskini ambaye hata pesa ‘tuition’ hana.”

”Mwalimu mmoja anaweza kufundisha nchi nzima kama ikifungwa hii ‘system’, wanafunzi watakuwa wanaonana na mwalimu na watakuwa ‘live’ na hata kuulizana maswali.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW