Habari

Meya Sitta atangaza neema kwa wavuvi Kinondoni (Video)

Meya wa Manispaa wa Kinondoni Mh.Benjamin Sitta amezindua rasmi maadhimisho ya siku ya wavuvi dunian ambapo amewaasa wavuvi hao kuepuka uvuvi haramu.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika soko la samaki Msasani wilayani humo ambapo kilele chake kitaifa itafanyika Jijini  mwanza hapo kesho.

Meya wa Halmshauri ya Kinondoni, Benjamin Sitta akizungumza na Wavuvi na wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki Msasani,Leo wakati wa uzinduzi wa siku ya wavuvi duniani

Katika hotuba yake sita amewataka wavuvi kuwafichua watu wanaojihusisha na uvuvi haramu hasa wanao tumia mabomu na baruti badala yake watumie uvuvi wenye tija.

Amesema serikali  ya manispaa na mkoa wanakuja na mkakati kabambe wa kudhibiti uvuvi haramu katika ukanda wa bahari ya hindi.

Afisa Uvuvi wa Manispaa ya Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza kwenye tukio hilo.

Lakin amesema manispaa yake inamkakati mzuri  wakuboresha miundombinu ya soko la samaki msasani ili liwe na hadhi ya kimataifa ambapo itaongeza kipato kwa wavuvi na wauzaji wa samaki.

Nae afisa wa Manispaa  Bi Grace Kakama Amesema wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na wavuvi katika kuhakikisha wanalinda Rasilimali za uvuvi zilizopo katika ukanda huo wa kinondoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents