Habari

Meya wa Kinondoni awapiga msasa Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji (Video)

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amefungua semina ya siku mbili kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na Watendaji wa Kinondoni ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi na kupunguza migogoro ambayo inatokea katika maeneo mbalimbali ya Kinondoni.

Awali ya hayo Sitta alisema Kinondoni ni sehemu ambayo inaongoza kwa migogoro mingi ya ardhi huku akidai mingi kati hiyo inasababishwa na Wenyeviti ambayo hawatambui majukumu yao.

Akizungumza na Wenyeviti hao katika ufunguzi wa semina hiyo, Sitta alidai tayari kuna Mtendaji mmoja ametimuliwa baada ya kusababisha matatizo katika mtaa wake.

“Semina hii ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mtaa na Watendani imezaliwa ndani ya kampeni ya Dar Mpya ya RC Makonda, sisi tumetumia fursa hiyo tukaamua kuwakusanya hawa ndugu zetu na kuwapa elimu ya utawala bora pamoja na kuwakumbusha majuku yao,” alisema Sitta.

“Hivi karibuni kuna Mtendaji ametimuliwa kutokana na utendaji mbaya, sasa sisi hatuishii kuwafukuza tu, kwa wale ambao watafanya vizuri tunaangalia namna ya kuwapatia zawadi ili waone kile wanachokifanya ni kikubwa sana. Kwahiyo semina hii bika shaka itawajengea uwezo na kupinguza baadhi ya migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza na kutia serikali hasara kwa sababu mpaka sasa tunadaiwa zaidi ya bilioni 10 zilisababishwa na wenyeviti wabovu,”

Meya alisema semina hiyo itaendeshwa katika kila wilaya ya ndani ya mkoa wa Dar es salaam ili kujenga taswira ya mpya ya uwajibikaji kuanzia ngazi ya mtaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents