Aisee DSTV!

Mfahamu ‘Christiano Ronaldo’ wa Atletico Madrid, asajiliwa kwa pauni Mil 113

Joao Felix sasa ndiye mchezaji ghali zaidi mwenye umri mdogo duniani baada ya kujiunga na Atletico Madrid kutoka Benfica kwa dau la pauni milioni 113.

 

Pia ametajwa kuwa mchezaji mahiri zaidi kutoka Ureno na kulinganishwa na Cristiano Ronaldo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alianza kuichezea Benfica mwanzoni mwa msimu wa 2018-19 lakini alifunga magoli 15 na kutoa pasi tisa zilizozaa magoli katika ligi hiyo ya Primeira huku klabu yake ikishinda taji la ligi.

Alifunga hat-trick dhidi ya klabu ya Ujerumani ya Eintracht Frankfurt katika ligi ya Yuropa mnamo mwezi Aprili , na kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika klabu ya Benfica na Ureno kufunga magoli matatu barani Ulaya mbali na kuwa mchezaji mdogo zaidi kufanya hivyo katika mashindano hayo.Felix alishinda taji la ligi na Benfica msimu uliopitaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kipaji chake kilimfanya kuitwa katika timu ya taifa ya Portugal na mara tu akaanza kuhusishwa na uhamisho wa klabu kama vile Manchester United na Manchester City kabla ya Atletico Madrid kumnunua kwa donge nono na kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi baada ya mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.

Bernardo Silva ndiye mchezaji bora duniani kwa sasa, alisema mkufunzi wa Swansea Carlos Carvalhal akizungumza na BBC Sport.

Lakini katika umri wa miaka 19 , hakuweza kuonyesha kipaji kama kile ambacho Felix anaonyesha akiwa na umri wa miaka 19 – hivyobasi fikiria ni mchezaji wa aina gani tunayezungumzia.

Ilikuwa wazi kwamba alikuwa ndiye mchezaji aliyekuwa na kipaji bora zaidi akiwa shule ya mafunzo ya soka.

Felix alianza kusakata soka katika timu ya vijana ya klabu ya Porto lakini aliwachiliwa 2015 , kwa madai ya kuwa mwembamba sana na kujiunga na wapinzani wao.Akiwa Benfica na umri wa miaka 16 alifanikiwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa wachezaji wa ziada kuwahi kuichezea klabu hiyo wakati alipoanzishwa mwezi Septemba 2016.

Akiwa Benfica na umri wa miaka 16 alifanikiwa kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi miongoni mwa wachezaji wa ziada kuwahi kuichezea klabu hiyo wakati alipoanzishwa mwezi Septemba 2016.

Lakini katika msimu wa 2018-2019 alianza kucheza rasmi na mnamo mwezi Novemba aliweka kandarasi mpya ilioshirikisha dau la kumnunua la Yuro 120m ambalo Atletico waliweza kulipa.

Mechi yake ya kwanza ilikua dhidi ya Boavista mnamo mwezi Agosti na katika mechi ya pili alifunga goli lake la kwanza dhidi ya wapinzani wao Sporting Lisbon kupitia kichwa kunako dakika ya 86 baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada.

Kushiriki kwake kulipungua chini ya mkufunzi Rui Vitoria lakini alichezeshwa mara kwa mara chini ya mkufunzi Bruno Lage ambaye alichukua ukufunzi wa klabu hiyo mwezi Januari – akifunga mara mbili katika mechi ya kwanza ya Lage na kumaliza msimu akiwa na magoli 20 kutoka mechi 43 katika mashindano yote.

Miongoni mwa vijana katika ligi kuu barani Ulaya – Uingereza, Itali, Uhispania, Ujerumani, Ufaransa , Ureno na Uholanzi – Felix alikuwa wa pili katika ufungaji wa magoli nyuma ya kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 19 Kai Havertz.Joao Felix sasa ndiye mchezaji ghali zaidi mwenye umri mdogo duniani

Na yuko nyuma ya winga wa Uingereza na Borussia Dortmund Jadon Sancho kwa upande wa magoli aliyochangia.

”Ndani ya klabu ya Benfica ilikuwa wazi kwamba alikuwa mchezaji bora zaidi katika shule ya mafunzo ya soka” , alisema Carvalhal.

Mabadiliko ya kuwa mchezaji wa kulipwa sio rahisi , lakini kwake ilikuwa rahisi. Wakati unapokutana naye nje ya uwanja , zungumza naye, mtazame akizungumza katika vyombo vya habari utagundua mvulana mwenye furaha.

Shinikizo ya kutaka kushinda ni kitu anachokabiliana nacho vizuri kila siku.

Jose Delgado, naibu mkurugenzi katika gazeti la Portuguese A Bola alimmiminia sifa chungu nzima kijana huyo.

”Tangu Ronaldo hatujawahi kuwa na mchezaji anayechangamsha na kijana kama yeye”, aliambia BBC Sport.

Ni Bora kuliko Silva katika umri wake.Anafananishwa na mchezaji wa zamani wa AC Milan na Brazil KakaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Felix atalinganishwa na wachezaji bora Ureno kwa sasa – mshindi mara tano wa tuzo la Ballon d’Or Ronaldo na Kiungo wa kati wa Manchester City Silva. Lakini mara nyingi hufananishwa na mshambuliaji wa zamani wa AC Milan na Brazil Kaka.

”Tayari wamemuita mrithi wangu ama Kaka mpya”, alisema mchezaji wa zamani wa Benfica na Ureno Rui Costa. ”Kusema kwali Felix ni Felix”.Felix lishinda taji la ligi na klabu ya benfica katika msimu wake wa kwanzaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ana uelewa usio wa kawaida wa mchezo mbali na uwezo wa kujua ni eneo gani analofaa kuwa mbele ya goli.

Carvalhal aliongezea: Tabia yake inafanana kama ile ya Kaka kwa maono yangu, vile anavyotamba na mpira, anavyowasiliana na wenzake na magoli yake.

Kwa nini yeye ni maalum?Felix anadaiwa mchezaji ambaye anafuata nyayo za Christiano Ronaldo

Ni mchezaji mwenye mchanganyiko wa kucheza namba 9 na 10 , anacheza kama mshambuliaji wa pili. Ni mchezaji mwenye vichwa vizuri hata iwapo sio mchezaji mwenye maungo makubwa.

Ni mchezaji anayejua kutafuta nafasi katika safu ya ulinzi ya upinzani, na ndio sababu yeye hufunga sana na hupiga mpira kwa kutumia migu yote miwili.

Wakati anapolazimika kucheza kati ya washambuliaji na viungo wa kati yeye ni gwiji.

Ni mchezaji mzuri mwenye ufundi. Kile kinachomfanya kuwa tofauti ni mshambuliaji anapowasili katika lango la upinzani na anafunga magoli.

Lakini pia ni mchezaji mzuri katika wingi katika kusaidia na kutoa pasi.

Akizungumza mnamo mwezi Mei, kabla ya Felix kujiunga na Madrid, Carvalhal aliongezea: Hio ndio maana sisi huzungumzia kuhusu klabu kubwa kuwa na hamu naye . Sio kitu cha kushangaza kwangu kwa sababu tangu mwanzo tumemuona kuwa mchezaji mwenye kipaji. Akiwa na umri wa miaka 19 anahitaji kukuwa na kujifunza.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW