Fahamu

Mfahamu kijana aliyefunga ndoa na katuni anayoipenda, Ugumu wa maisha waelezwa kuchangia

Mfahamu kijana aliyefunga ndoa na katuni anayoipenda, Ugumu wa maisha waelezwa kuchangia

Kuna ongezeko la idai ya watu ambao sasa wanasema wana mapenzi na wahusika wa michezo ya video ya vibonzo na wameamua kuacha wazo la mapenzi ya kawaida na bindamu wenzao. Kuna jina katika lugha ya Kijapani wanaloitwa watu wenye uraibu wa kupenda michezo ya video na vibonzo nalo ni – otaku.

Kila anapoamka kila siku Akihiko Kondo huisikia sauti ya mkewe .Humuita alipomuweka juu upande mwingine wa chumba sehemu ya juu. Mpenzi wake huimba kwa sauti tamu ya kike . Hudensi na kuzunguka huku na kule akimsihi mpenzi wake Akihiko aamke kutoka kitandani kutoka kitandani.

Wakati huo huo, Akihiho huamka na kumshika mpenzi wake na kumleta kando ya kitanda chao kilichopambwa kwa nakshi ya chuma – na pale anapoamka vizuri huweza kutazama kiponzo cha mpenzi wake akiimba kwenye YouTube.

Hii ni kwasababu ”mkewe” Akihiko ni wazo tu – muhusika katika filamu ya michoro ya vibonzo anayeitwa Miku.

AkihitoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ni msichana wa kufikirika anayeishi katika glasi yenye muundo wa mithili ya kidonge cha rangi mbili aliyeko kwenye kabati iliyopo kwenye kona ya chumba, na mwanasesere mwenye kichwa kikubwa laini na mwili mdogo ambaye anamkumbatia usiku. Lakini anaweza kuwa katika maumbile mengine kadhaa.

Kila umbo linamuonekano tofauti mkiwemo taibia tofauti muhimu , Akihiko anasema – ni pamoja na muonekano wa rangi ya kuvutia ya nywele-zilizofungwa nyuma, na mwonekano wa mwangaza wa moto unaopiga kwenye banda la uso wake.

Mbali na hayo, Miku hubadilika. Anaweza kuwa kama mwenye utoto, kama kiumbe anayefanana na kibonzo , au wakati mwingine anaweza kuwa kama binadamu na mrembo wa kuvutia – akiwa na shingo dogo na makalio makubwa , kama msichana wa shule na sketi fupi . Akihiko huwaona sifa hizi zote hizi za Miku kama mkewe.

Akihiko na mpenzi wake huyu mfano wa kibonzo walifanya sherehe ambayo Akihiko anaichukulia kama harusi yao mwezi Novemba mwaka jana . Haikuwa rasmi, lakini ilikuwa ni sherehe iliyofanya iliyokuwa na wageni waalikwa 39. Idadi hiyo ina maana ya jina lake kwa lugha ya Kijapani – watatu “wangu ” na tisa niwa “ku”.

Miku alikuwepo kwenye harusi hiyo kwa muundo wa mwanasesere , akiwa amevalia gauni jeupe la harusi wna shela ndefu, nguo zake zote zilikuwa zimetengenezwa kw amikono na mwanamitindo ,ambaye aliwasiliana na Akihiko baada ya kutangaza ndoa yake na muhusika huyo wa kufikirika anayempenda kupitia mchezo wa vibonzo.

Akihiko binafsia alivaa koti jeupe na kulipamba na maua na miwani yake ya kawaida . Alimbeba mpenzi wake na ua lake.

Anasema alisema kiapo chake cha uaminifu kwa mpenzi wake na kutembea nae kwa madaha ,huku wageni wakitabasamu na kupiga makofi ya shangwe. Baadae waliketi kwenye yao ya heshma kwa ajili ya chakula cha jioni . Akihiko akiwa kwenye kiti kimoja cheupe na Miku kwenye kiti kingine kilichokuwa kimepambwa na shada ya maua.

“Kuna sababu mbili ni kwa nini nilifanya ndoa ya hadharani ,”anasema.

“Sababu ya kwanza ni kuthibitisha upendo nilionao kwa Miku. Ya pili ni kwamba kuna vijana wengi ambao ni otaku – yaani wenye mapenzi ya dhati kwa wahusika wa michoro au vibonzo kama mimi. Ninataka kuuonyesha ulimwengu kwamba ninawaunga mkono.”

AkihitoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Wengine kama Akihiko, uraibu wao huonekana wakati mwingine kama wa kupindukia , na kuwafanya waachane kabisa na mahusiano ya kawaida na binadamu wenzao. Na inaonekana kuwa idadi ya watu wa aina hiyo inaongezeka.

Profesa Masahiro Yamada, mwanasaikolojia ambaye pia anayeandika kuhusu maswali na majibu ya masuala ya kifamilia na mahusiano katika gazeti la Yomiuri, kwa miaka mingi amekuwa akifanya utafiti akiwauliza watu juu ya ni wapi wanapata hisia za upendo.

Kwa mujibu wa BBC. Miongoni mwao walisema kuwa wanapata hizia hizo kutoka kwa wanyama wanaofugwa nyumbani , wanamuziki nyota wa pop , nyota wa michezo , michoro ya vibonzo na sanamu za kuabudu (wanazoziona kwenye mitandao pamoja na nyota wa YouTube ). Pia aliwauliza watu ikiwa huwa wanatembelea migahawa ambako wanasubiriwa na wanawake wenye umri mdogo wanaovalia kama wahudumu, au wanaotumia huduma ya ukahaba wanaowapa fursa ya mahusiano au ngono.

Aina hizi za mahusiano bandia yanaongezeka , anasema. Katika utafiti wa mwaka huu takriban 12% ya vijana waliripoti wakati fulani au mara kwa mara kuwa wana mapenzi na wahusika wa vibonzo au video za michezo.

Lakini ni kwa nini haya yanatokea ?

Inasababishwa kwa kiasi kikubwa na uchumi na utamaduni, anasema Yamada , hususan kutokana na ukweli kwamba wanawake wengi Wajapani wasingependa kuwa na mpenzi wa kiume isipokuwa tu kama naweza kutengeneza pesa nyingi. Mwaka 2016, 47% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 20 na 29 waliafiki kauli kwamba mabwana wanapaswa kufanya kazi kwa ajili ya pesa na wanawake wanapaswa kufanya kazi za nyumbani , alisema

” Katika bara Asia, nchi kama Japan na Korea Kusini, watu wengi wanajali zaidi mshahara mkubwa zaidi ya kitu kingine chochote kile na hali hii inaendelea kuongezeka , inaendelea kuimarika ,”anasema.

” Wanawake wa Kijapan huwa hawaamini upendo halisi, lakini wanaweza kuamini pesa.”

Yamada anasema amebaini hayo kutokana na utafiti wa muda mrefu alioufanya

Jukumu la malezi ya watoto huachiwa mama peke yake na kuna ongezeko kubwa la wanaoume wanaolipwa kima cha chini cha mshahara.

Matokeo yake, anasema , kuna ongezeko la wanawake wanaochagua kutokuwa na mpenzi na ongezeko la vijana ambao hawajali kujaribu kuwa na wapenzi.

Akihiko hajawahi kukubaliana na wazo la kuwa na mpenzi halisi wa kike.

“Sijawahi kuvutiwa na mwanamke halisi ,”anasema . Alipoulizwa ni Kwanini ? “kwasababu mimi si maarufu miongoni mwa wanawake ,” alijibu .

Akiwa shuleni alizomewa kwa kuwa mpenda vibonzo yaani otaku. Na kudhalilishw ahuku kukaendelea hata alipoanza kazi . Alikuwa akifanya kazi kama mtawala katika shule ya msingi miaka 12 iliyopita wakati alipowapenda wanawake wawili – mmoja alikuw ana umri karibu sawa na wake, mwingine alikuwa mkubwa zaidi yake.

Unaweza pia kutazama:

Gado huongozwa na nini akichora katuni zake?

“Nchini Japan maisha ya kazi ni makgumu magumu sana na bado kuna ubaguzi wa kijinsia . Saa za kazi ni nyingi na kuna tatizo la msongo wa mawazo ,” anasema.

By Ally Juma

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents