Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mfahamu kinda wa miaka 16 anayeumiza vichwa Mabosi wa Dortmund, Liverpool, United na Chelsea, wengine sokoni

Borussia Dortmund wanazidi kuwapiku Liverpool, Manchester United na Chelsea kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England kwa vijana walio na umri chini ya miaka 17, Jude Bellingham

Image result for jude bellingham

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 16, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Birmingham City F.C inayoshiriki EFL Championship (Bild, in German)

Manchester City, Juventus na Paris St-Germain wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem Aouar, mwenye umri wa miaka 21, kutoka klabu ya Ufaransa ya Lyon. (Corriere dello Sport, in Italian)Jude Bellingham anasakwa na timu tatu za EnglandJude Bellingham anayesakwa na timu tatu za England

Arsenal wamefanya mazungumzo na Hammarby juu ya kusainiwa kwa mkataba na mchezaji kutoka kikosi cha kimataifa cha vijana wadogo cha Sweden Emil Roback, mwenye umri wa miaka 16, anayecheza skatika safu ya kati ya mashambulizi ambaye pia Bayern Munich wameonyesha azma ya kutaka kumnunua. (Daily Mail)

Arsenal pia watafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Villarreal Santi Cazorla katika msimu huu ili kumpatia fursa ya kusema kwaheri kwa mashabiki wake. Muhispania huyo mwenye umri wa miaka 35-aliondoka Gunners katika msimu wa majira ya joto wa mwaka 2018,baada ya kutocheza mechi kwa karibu miaka miwili kwasababu ya jeraha alilokuanalo. (Daily Express)Manchester City, Juventus na Paris St-Germain wote wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem AouarManchester City, Juventus na Paris St-Germain wote wameonyesha nia ya kusaini mkataba na kiungo wa kati Mfaransa Houssem Aouar

West Ham wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kimchezo ya difenda Muingereza Dion Sanderson, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika Cardiff kutoka Wolves. (Daily Mail)

Chelsea wamezungumza na Barcelona kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo msimu ujao. (Sport, in Spanish)

Manchester City na Manchester United wako tayari kumchukua kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, huku kijana huyo mwanye umri wa miaka 25- akihangaika kusaini mkataba mpya na Atletico Madrid. (Mundo Deportivo, in Spanish)Mbrazil Philippe Coutinho huenda akachukuliwa na BarcelonaMbrazil Philippe Coutinho huenda akachukuliwa na Barcelona

Inter Milan wako tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja zaidi Muingereza Ashley Young, mwenye umri wa miaka 34, baada ya kuwafurahisha kimchezo tangu alipohamia kikosini mwezi Januari kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport, in Italian)

Shirikisho la soka la Ireland linamtaka meneja wa Stoke Michael O’Neill kuendelea kuongoza mechi za timu ya taifa ya Ireland Kaskazini kwa ajili ya Euro 2020, ambazo zimeahirishwa hadi Juni kwasababu ya janga la coronavirus. (Daily Mirror)Mjamaica Leon Bailey anafuatiliwa na Arsenal na Chealsea

Mjamaica Leon Bailey anafuatiliwa na Arsenal na Chealsea

Dau la Aston Villa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Angers Baptiste Santamaria lilikataliwa mwezi Januari na bado hawajaamua ikiwa watatoa pesa zaidi kwa ajili ya kijana huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 25-msimu huu. (ABC Sevilla, in Spanish)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW