Aisee DSTV!

Mfahamu kinda wa Senegal na ‘Man of the match’ dhidi Taifa Stars, anayekipiga na Samatta, kuhusishwa na Man United (+Audio)

Timu ya taifa ya Senegal hapo jana ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Tanzania katika mchezo wa michuano ya Afcon kwa mwaka huu inayoendelea kushika kasi huko nchini Misri.

Miongoni mwa mabao hayo mawili yaliyofungwa Senegal moja limewekwa kimyani na kinda wa miaka 20, Krepin Diatta ambaye alilifunga bao hilo safi kwa shuti kali katika dakika ya 65 amabalo kipa wa Tanzania Aishi Manula lilimshinda kulizuia na kulisindikiza kwa macho mpaka nyavuni.

Umiliki wa mpira baada ya dakika 90 ulisalia kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza, Senegal 61% na Tanzania 39%. Wakati kwenye mashuti langoni, Senegal wamepiga michomo 23, kati ka hiyo 13 ikilenga lango.

Hebu achia mbali mchezo huo, na turudi kwa mfungaji wa bao la pili, Krepin Diatta aliyeonyesha uwezo mkubwa katika mechi hiyo hadi kupelekea kuchaguliwa kuwa “Man of the match“ Senegal dhidi ya Tanzania.

Krepin Diatta ni nyota wa timu ya taifa ya Senegal ambaye amezaliwa Februari 25, 1999. Anayecheza nafasi ya ushambuliaji ndani ya Club Brugge ya Ubelgiji.

Club Brugge ambayo anakipiga Diatta ilimaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama First Division A ambayo inajumla ya klabu 16 huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na KRC Genk ya Mbwana Samatta na kutawazwa kuwa mabingwa.

Mwaka 2017, akiwa na umri wa miaka 18, Krepin Diatta tovuti ya Manchester Evening iliripoti kijana huyo kuhitajika na Manchester United na mwenyewe kukiri kufanya manao mazungumzo zaidi ya mara kadhaa.

Krepin Diatta alikuwa na ndoto za kucheza Manchester United baada ya kukutana na watu ‘ ma-scouts’ wa klabu hiyo, baada ya kupita miezi kadhaa chombo cha habari cha ESPN kiliripoti kuwa nyota huyo aliyekuwa akikipiga timu ya taifa ya Senegal waliyo chini ya umri wa miaka 20 alikuwa akifuatiliwa maendeleo yake.

Wakati huo kinda huyo alikuwa kiitumikia klabu ya Sarpsborg 08 ya Norway, United waliamini wanaweza kufuatilia uwezo wake pindi atakapoikabili timu ya Odds Ballklubb.

Nyota huyo aliyebarikiwa kipaji katika kupiga mipira iliyokufa ‘pace’  alifanya mazungumzo na ‘scouts’ zaidi ya mara mbili baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 20. Aliwahi kukiambia chombo cha habari cha TV2 kuwa ameshafanya mazungumzo na ‘scouts’ wa United zaidi ya mara mbili.

“Sikufahamu kuwa Manchester United wananifuatilia, lakini kujiunga nayo ni ndoto ambazo zitakuja kutimia. Nafikiri niko vizuri, lakini kwa sasa anichezea Sarpsborg na naipenda hii klabu. Tutafahamu hapo baadae nini kitakuja kutokea.”- Krepin Diatta aliwahi kusema kwenye mahojiano hayo akiwa na umri wa miaka 18.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW