Tupo Nawe

Mfahamu kocha aliyependekezwa na Sir Alex Ferguson kuifundisha Manchester United

Aliyekuwa kocha wa miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri muda wowote huwenda akatua katika Premier League.

Massimiliano Allegri is a man in demand after stepping down as Juventus boss in the summer

Muitalia huyo hivi karibuni ameonekana uwanjani akishudia mechi ya Tottenham dhidi ya Bayern Munich ambayo vijana wa Spurs wakikubali kipigo cha mabao 7 – 2 na kuzua maswali kama huwenda akatua kuchukua nafasi ya  Pochettino ambae amehusishwa kuondoka.

Manchester United siku zote imekuwa ikivutiwa na Allegri ambaye mwaka huu 2019 ameacha kuifundisha Juventus kwa kushindwa kuipatia ubingwa wa Ulaya baada ya kuichukua timu hiyo tangu mwaka 2014.

Aliyekuwa Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson aliwahi kumpendekeza kocha huyo, Allegri tangu mwaka 2013 kuwa mbadala wa David Moyes kisha Louise van Gaal na hata Jose Mourinho ili kuja kukijenga upya kikosi hicho cha United.

Man United, who are struggling under Ole Gunnar Solskjaer, have always fascinated Allegri

Ferguson anavutiwa na Ole Gunnar Solskjaer lakini pia amekuwa akiikubali kazi kubwa iliyofanywa na Allegri baada ya kushinda mataji matano ya Serie A akiwa na Juve.

United ipo katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Premier League, ikiwa na pointi tisa ikishinda michezo miwili (2), ikifungwa mitatu (3) na sare tatu (3).

Matokeo hayo ya United ikiwa imeshacheza michezo nane (8) mpaka sasa, kocha Solskjaer anakabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Liverpool huku kama atapoteza basi kibarua chake kitakuwa mahala pabaya zaidi.

Legendary United manager Sir Alex Ferguson is a man Allegri looks up to

Allegri ni muumini wa mfumo wa 3-5-2,  4-4-1-1,  4-3-3 na 4-2-3-1 lakini pia nimaarufu kwa kuendana na aina ya staili ya uchezaji wa wapinzani wake pindi timu inapokuwa katika presha.

Kocha, Allegri amekuwa akisifika kwa kuwa na mahusiano mazuri na wachezaji wake, na huwenda hiyo ikawa ndiyo sababu ya yeye kupata mafanikio makubwa katika michuano ya Ulaya kwa kuifikisha Juventus hatua ya fainali ya Champions League mara kwa mara, ikipoteza na Barcelona mwaka 2015 miaka miwili baadaye na Real Madrid.

Kuanzia msimu wa mwaka 2014/19 akiwa na Juventus akibeba ubingwa wa Serie A  mara tano. 4 Italian Cups, 2 Italian Super Cups.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW