Fahamu

Mfahamu kwa ufupi rapper Nipsey Hussle, aliyepigwa risasi nje ya duka lake hadi kufa Los Angeles nchini Marekani

Wengi wakimjua kama Nipsey Hussle lakini jina lake la kuzaliwa likiwa ni Ermias Joseph Asghedom aliyezaliwa miaka 33 iliyopita August 15, 1985 kusini mwa Los Angeles nchini Marekani na kupoteza maisha yake March 31, 2019 (aged 33) Los Angeles, California, U.S.A ikiwa ni nje ya duka lake la nguo.

Baada ya kupoteza maisha Wasanii maarufu nchini Marekani wakiwemo Drake, Rihanna na J Cole wametoa rambi rambi zao kufuatia kifo cha rapa wa Los Angeles Nipsey Hussle, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mjini humo.

Msanii huyo wa miaka 33 alipigwa risasi nje ya duka lake la kuuza nguo.

Drake alimuelezea marehemu kama “mtu maarufu mwenye heshima”, huku Rehanna akiandika katika mtandao wake wa Twitter: “Hii haingii akilini, Nimeumizwa sana na tukio hili!”

Watu wengine wawili walijeruhiwa katika kisa hicho cha ufyatulianaji risasi kilichotokea nje ya duka la Marathon kusini mwa mji wa Los Angeles.

Luteni kanali Chris Ramierez wa kitengo cha polisi cha Los Angeles ameambia vyombo vya habari katika eneo la tukio kuwa mshukiwa aliyetekeleza uhalifu huo alionekana kama mwanamume mweusi.

Albamu ya kwanza ya msanii Nipsey Hussle, kwa jina ”Victory Lap” aliteuliwa kuwania albamu bora ya mwaka ya muziki wa rap katika tuzo ya Grammy.

Wasanii wengine ambao waliteuliwa kuwania tuzo hiyo ni pamoja na Cardi B, Mac Miller, Pusha T na Travis Scott.

Katika Instagram yake, Pusha alimtaja kama “mtu wa aina yake “: “Inasikitisha kuwa umetutoka Nip, napata faraja nikiwa na fahamu kuwa umebarikiwa… Nilipata heshima ya kutangamana nawe mwaka mzima kupitia sanaa yetu ya muziki.

Drake, ambaye alishinda Grammy kutokana na kibao chake Killer Nipsey Hussle 2009, pia alitoa rambi rambi zake kwa marehemu.

“Nimeishiwa na ngavu kabisa baada ya kupokea taarifa za kifo chako,” aliandika. “Tuliwasiliana mara ya kwanza baadaya miaka mingi na tukakubaliana kutoa wimbo mpya hivi karibuni kwasababu imetuchukua muda mrefu kufanya hivyo.

“Ulikuwa unafanya vizuri na lilikuwa nikijivunia ufanisi wako na kukufuatilia kwa karibu, hakuna mtu yeyote aliyetaja jina lako kwa ubaya, ulikuwa mkweli katika mahusiano yako na watu na kwetu sote.”

Wengine waliyotuma rambi rambi zao ni pamoja na rappa J. Cole na mtayarishi na msanii Pharrell Williams.

https://twitter.com/Pharrell/status/1112510612448243712?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1112510612448243712&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.bbc.com%2Fswahili%2Fhabari-47774974

Meya wa jiji la Los Angeles, Eric Garcetti, alisema kifo cha Hussle ni “pigo kubwa”.

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Clippers jijini Los Angeles Montrezl Harrell aliandika rambi rambi zake katika kiatu chake cha mazoezi.

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya LA Clippers Montrezl Harrell aliandika kuhusu kifo cha Nipsey katika kiatu chake cha mazoezi
Image captionMchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya LA Clippers Montrezl Harrell aliandika kuhusu kifo cha Nipsey katika kiatu chake cha mazoezi

Jina halisi la Hussle, ni Ermias Davidson Asghedom, alikulia kusini mwa Los Angeles na alikuwa mwanachama wa kundi la mtaani lililofahamika kama Rollin’ 60s alipokuwa kijana mdogo.

Baadaye alikuwa mshirikishi wa masuala ya kijamii na alijihusisha na mradi wa sanaa wa Crenshaw.

“Nilikuwa katika utamaduni wa magenge,”aliambia gazeti la Los Angeles Times mwaka 2018. “Tulishuhudia vurugu na mauaji. Ilikuwa sawa na kuishi katika eneo la vita, ambako watu wanafariki kala mara na wakaaazi walikuwa wamezoea kuishi katika mazingira hayo”

Mapema Jumapili, aliandika katika Twitter: “Kuwa na maadui ni baraka.”Ruka ujumbe wa Twitter wa @NipseyHussle

THA GREATāœ”@NipseyHussle

Having strong enemies is a blessing.314K12:52 AM – Apr 1, 2019Twitter Ads info and privacy184K people are talking about this

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @NipseyHussle

Safari ya maisha ya Nipsey mitaani hadi kufikia umaarufu wake

Katika maisha yake ya muziki, Nipsey Hussle alisisitiza umuhimu wa mtu kuwa huru kiuchumi na iliajiendeleze maishani.

Ilimchukua miaka 10 kutoa albamu yake ya kwanza, kwa jina Victory Lap, na alikataa ufadhili wa lebo kubwa duniani na kujenga himaya yake kuanzi chini.

Ilipata umaarufu kwa, kuuza nakala 1,000 ya mchanganyiko wa nyimbo zake kwa jina Crenshaw mwaka 2013 ambapo alijizolea $100 – na hata kumshawishi Jay-Z kununua nakala 100.

Hatua ambayo ilimwezesha kujiimaraisha kifedha na kuendelea na tasnia yake ya muziki.C

Hussle hakuwahi kuficha ukweli kuwa aliwahi kuwa mwanachama wa genge hatari la Rollin’ 60s, lakini sauti yake ya kipekee na maudhui ya tungo zake kuhusiana na visasa vya mauaji kuw kutumia bunduki na matumizi ya mihadarati mara nyingi iliwagusa wale waliyokuwa wakitekeleza uhalifu.

“Mimi kuwa na utu ni jambo la kwanza kabla ya kuwa msanii,” aliambia Billboard mwaka jana. “Nataka kuleta mabadiliko kwa kubadilisha hali ya maisha katika jamii niliyokulia ndani, na nyingine sawia na hiyo.”

hapo jana baada ya Idara ya polisi mjini Los Angeles kutoa jina la mshukiwa mmoja (Eric Holder) ambaye anatuhumiwa kuhusika kufyatua risasi na kumuua Nipsey.

Kwa mujibu wa maelezo yao ni kwamba Eric (29) anahusika kwa mauaji hayo pamoja na wengine wawili waliopoteza uhai kwenye shambulio hilo. Eric Holder, mtuhumiwa wa mauaji ya rapper #NipseyHussleamekamatwa, polisi wamemtia nguvuni

By Ally Juma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents