Habari

Mfahamu Mfalme wa Kondomu, anayehamasisha watu kutumia ili kujikinga dhidi ya maambukizi ya HIV

Stanley Ngara, anayefahamika kwa jina maarufu kama mfalme wa kondomu Kenya, amekuwa akisambaza mipira ya kondomu katika jiji la Nairobi, kwa lengo la kuhamasisha watu umuhimu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi(VVU).

Stanley Ngara

Leo ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi dunini, shirika la habari la EPA linaripoti kuhusu mfalme huyu wa aina yake.Stanley Ngara

Stanley Ngara maarufu mfalme wa Kondomu

“Mipira ya kondomu imehusishwa na uasherati kwa sababu watu hufikiria kuwa mtu akiwa ameathirika na ugonjwa huo basi yeye ni kahaba au anashiriki ngono na zaidi ya mtu mmoja,” aliliambia shirika la habari la Bloomberg agency.

Mfalme huyo anajaribu kukabiliana na dhana hiyo potofu inayosababisha unyanyapaa.Stanley Ngara

Stanley Ngara, amekuwa akitumia nafasi ya kusambaza mipira ya kondomu jijini kuhamasisha umuhimu wa watu kijikinga dhidi ya maambukizi ya HIV

Akishirikiana na washika dau wengine Bw,Ngara huzungumzia maambukizi ya VVU na Ukimwi, suala ambalo anasema bado halizungumziwi hadharani.

Amekuwa akishirikiana na wadau wengine kuangazia Ukimwi na maabukizi suala amabalo bado halizungumziwi hadharani

Amekuwa akishirikiana na wadau wengine kuangazia Ukimwi na maabukizi suala amabalo bado halizungumziwi hadharani

“Kenya inahitaji wafalme na malkia wengi zaidi wa mipira ya kondomu,” mwanaharakati huyo wa mika 47-aliiambia shirika la habari la EPA."Kenya inahitaji wafalme na malkia wengi zaidi wa mipira ya kondomu"

Kenya inahitaji wafalme na malkia wengi zaidi wa mipira ya kondomu,”

Umoja wa mataifa unasema kuwa karibu watu milioni 1.6 nchini Kenya wanaishi na virusi vya ukimwi tangu mwaka 2018 huku wengine 25,000 walifariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.

Japo hatua kubwa imepigwa kukabiliana na ugonjwa huo katika miaka ya hivi karibuni, suala la unyanyapaa dhidi ya ugonjwa huo zinalemaza juhudi za kudhuibiti maambukizi, mkuu wa UNAids Winnie Byanyimaa aliiambia BBC.Stanley Ngara: Mfalme wa Kondomu wa Kenya anayekabiliana na maambukizi ya Ukimwi

Stanley Ngara: Mfalme wa Kondomu wa Kenya anayekabiliana na maambukizi ya Ukimwi

“Tunahofia huenda tukapoteza mapambano dhidi ya unyanyapaa, kwa sababu vijana ambao wamepatikana na virusi vya ukimwi-hawajitokezi kutafuta matibabu kwa kuhofia kuhukumiwa… kwasababu UKIMWI bado inachukuliwa kama dhambi, alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents