Habari

Mfahamu mkulima wa Konokono kwaajili ya chakula, adai wana ladha nzuri na watamu

Taylor Knapp anasema kuwa anaona konokono ni wazuri kabisa kutokana na usimamizi wake wa konokono zaidi ya 70,000

konokono

Bwana Knapp ni mwazilishi na mmiliki wa shamba kubwa zaidi la konokono nchini Marekani, kuna mashamba mawili tu ambayo yamepitishwa na taasisi ya kusimamia kilimo (USDA)

Anapeleka konokono kwenye migahawa ya New york na anajitahidi kuhakikisha anapeleka wa kutosha lakini bado kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa hiyo. Amepata faida maradufu tangu aanze biashara hiyo mwaka 2017.

Bwana Knapp ana miaka 31, pia ni mpishi mashuhuri, alikuja na wazo hili baada ya kula konokono wanaotoka shambani moja kwa moja huko ulaya.

Unaweza pia kusoma

Anasema kuwa wana ladha nzuri sana na watamu kuliko wale waliohifadhiwa kwenye makopo ambao wanapatikana kwa wingi nchini Marekani.

Lakini anasema kuwa ni marufuku kwa migahawa ya Marekani kuingiza konokono wanaotoka shambani kutoka nchi nyingine iwe wamekufa au wazima bado. Na konokono aina tatu wanaofanywa kama chakula asili yao ni barani Ulaya.Taylor KnappTaylor Knapp ana mipango ya kuongeza wateja nje ya New York

Takwimu za biashara zinaonesha kuwa walaji wa konokono wameongezeka hadi asilimia 42 na tani 300 zikitumika kwa mwaka 2018. Baada ya hapo aliona fursa ya kibiashara na akaamua kuanzisha shamba lake ili kupata bidhaa safi zinazotoka shambani.

Konokono wa bwana Taylor Knapp amewatoa jimbo la California ambapo alinunua wachache kwa ajili ya kula na baadae akaanza kuwazalisha.

Konokono hao wana asili ya California tangu mwaka 1850 na baada kuletwa Marekani kutoka Ulaya na wahamiaji, inaonekana mhamiaji huyo alifanikiwa kuwapitisha katika mpaka bila kugundulika, mpaka huo uliokuwepo tangu mwaka 1789.

Unaweza pia kusoma:

Taylor na mshirika mwenzake walianza na mtaji wa dola za marekani 30,000 kutoka kwa michango ya watu na wawekezaji wengine, kisha wakaanza kufanya kazi kwa ukaribu na taasisi ya kilimo cha chakula.EscargotsEscargots ni aina ya konokono wanaweza kuwekwa kitunguu swaumu kwa ladha nzuri

”Ni kazi ngumu”, anasema Ric Brewer ambae ni mmiliki wa shamba jingine la konokono huko Washington.

”USDA inapanua vitendea kazi, wakaguzi wa kupitia mashamba ya konokono”anasema Brewer

Shamba lake lilifunguliwa mwaka 2011 na sasa lina konokono 50,000, na wengi wao ni aina ya wale wadogo wadogo.

”Ni chakula kizuri sana na hawana madhara kwenye mazingira, na wanapikwa kama ambavyo ungepika dagaa kamba ama kaa” anaongeza Brewer.konokono Peconic EscargotKonokono katika shamba la Peconic wanapata matunzo na kuwekea dawa

Rick na Taylor wote wanauza konokono wabichi, na wanaweza kudumu kwa wiki moja, hawa ni tofauti sana na konokono wanaowekwa kwenye makopo ambao.

Mpishi Ryan Angulo anasema kuwa konokono wa kutoka shambani ni wazuri sana kuliko kwenye makopo, ”wana ladha nzuri, na harufu nzuri”

kwasasa ni marufuku kusafirisha konokono wanalimwa shambani kwenda nje ya Marekani, hivyo ni vigumu kwa wakulima hawa kupanua soko lao.

”Konokono ni wazuri lakini siwezi kusema nawapenda, nikisema nawapenda nitakua nimeongeza chumvi” anasema Taylor.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents