BurudaniUncategorized

Mfahamu mrembo Miri Ben-Ari aliyeshirikishwa na Diamond kwenye Baila kupiga Violin

Miri Ben-Ari amejizolea umaarufu mkubwa Bongo baada ya kusikika katika albamu mpya ya Diamond, kupitia wimbo wa Baila ambao ameshirikishwa akiwa amepiga violini. Lakini wengi hapa Bongo bado hawamfahamu zaidi mrembo huyo kwenye muziki na wengine wamekuwa wakimchukulia poa.


Miri Ben-Ari

Miri alizaliwa Disemba 4, 1978 mjini Tel Aviv, lakini pia ni raia wa nchi mbili ambazo ni Israeli na Marekani.

Alianza kujifunza upigaji wa Violini akiwa na umri wa miaka 5 na alipofikia umri wa miaka 12. Wakati huo huo alichaguliwa na mkongwe wa upigaji violini Isaac Stern kwa ajili ya kutumbuiza pamoja kwenye sherehe za jeshi la Israel.

Baadae Miri alihama Israel na kwenda New York kwa ajili ya kujifunza Jazz kwenye chuo cha The New School, lakini alifukuzwa baada ya kusoma semesters mbili kutokana na mahudhurio mabaya yaliyosababishwa na kujikita zaidi kwenye mchezo wa Gigs ili aweze kujilipia kodi.

Mwaka 1999 mrembo huyo aliachia albamu yake ya kwanza ya ‘Sahara’ chini ya lebo ya Half Note Records. Lakini pia ana albamu nyingine nne ikiwemo ‘Temple of Beautiful’, ‘Live at the Blue Note’, ‘The Hip-Hop Violinist’ na ‘Song of the Promised Lan’.

Mwaka 2005 Miri alifanikiwa kushinda tuzo ya Grammy kupitia wimbo wa ‘Jesus Walks’ wa Kanye West ambao unapatikana kwenye albamu yake ya ‘The College Dropout’.

Mrembo huyo pia amewahi kufanya kazi na kutumbuiza katika jukwaa moja na mastaa wengi akiwemo Jay Z, Kanye West, Wyclef Jean, Alicia Keys, John Legend, T-Pain, Janet Jackson, Brandy, Akon na wengine.

Pia Miri Ben mwaka 2012 alialikwa na aliyekuwa rais wa Marekani, Barack Obama kutumbuiza ikulu.

                            Miri Ben-Ari akiwa na Barack Obama

Kwa Diamond kumshirikisha msanii huyo haikuwa kazi kubwa sana kumpata maana wote kwa pamoja wapo chini ya Universal Music Group.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents