Burudani

Mfahamu msanii huyu wa Burundi anayekuja kwa kasi

Ukiwataja wasanii wa muziki kutokea nchini Burundi, basi wanaofahamika watakuwa ni Kidum na Lolilo tu. Pamoja na kuwa ana makazi yake nchini Kenya,Kidum ni mzaliwa wa Burundi aliyewahi kutengeneza hit songs nyingi zilizotawala chati za radio na TV mbalimbali Afrika ya Mashariki.

Nyimbo kama vile ‘Nitafanya’ feat Jaydee, ‘Haturudi nyuma’ feat Juliana Kanyomozi ni baadhi ya nyimbo zake ambazo bado ni gumzo. Lolilo naye kwa upande wake, alijijengea jina Afrika Mashariki kupitia nyimbo alizowashirikisha Diamond na pia Alikiba. Ila kwa sasa Kazima.

Miongoni mwa wasanii wa muziki wanaojitahidi kuinua kiwanda cha muziki Burundi kilichoanza kuyumba miaka ya nyuma ni Nkejimana Herve aka Chris Dizzo. Mwaka 2005 akiwa bado mtoto alisafiri pamoja na nduguye South Africa alikopelekwa kwa ajili ya masomo. Kutokana na ndoto yake ya kuwa muimbaji alianza kujihusisha na muziki akiwa mdogo, ambapo baadaye akaja akakatisha masomo yake ili apate wakati mzuri wa kurekodi.

Mnamo mwaka wa 2008, Dizzo alipata nafasi ya kuingia studio kwa mara ya kwanza akarekodi single yake ya kwanza ‘Hafsa’ na baadaye ikafuata ‘step slow’ mwaka uliofuata, nyimbo ambazo hazikufanya vizuri kivile kule South na pia Burundi.

Kutokana na changamoto zilizomkabili, alirejea home na mwaka wa 2012 aliachia single nyingine ‘Incungu’ wimbo uliomtambulisha vizuri kwao Burundi na kumtengenezea jina. Aliweza kupata nomination ya Kora Awards katika kitengo cha ‘Best male East Africa’ akishindana na Redsan,Alikiba,Kidum na wengine.

Hatua ilimpa nguvu za kuendelea na aliweza kuungana na wasanii wengine kutoka Burundi kama vile;Big fariouz,Sat B,Yoya,Lolilo na Nkonmbozi ili kuweza kupiga hatua zaidi kimziki.

Kwa sasa, Dizzo anashughulikia album yake ya kwanza akiwa South Africa,huku akidhamiria kusaini mkataba wa kihistoria na lebo moja kubwa ya South ila amesita kuitaja jina kwa sasa. Ameahidi kwamba itakuwa ni album ya aina yake na itakuwa ndio mwanzo wa nyota yake kung’aa Afrika ya Mashariki na bila shaka kupata airplay.

Kuhusu msanii anayemkubali kutoka Afrika Mashariki,Chris Dizzo anamtaja Alikiba kama role model wake na kuwa ni mfano wa kuigwa na vijana wengi. Anaendelea kusema kuwa wimbo wa kiba ‘Mapenzi Yanarun Dunia’ ndio wimbo ambao utabaki kuwa kwenye playlist yake. Anasema anampenda Kiba na panapo majaliwa atamshirikisha kwenye iyo album yake.

Dizzo anaamini kwamba ana uwezo wa kubadilisha hali ya kiwanda cha mziki iliyodorora kwa sasa nchini Burundi.

Makala ya: Teddyza Agwa
Whats app:+254710487436

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents