Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Mfahamu mtangazaji aliyetokea kwenye video ya Bahati na Raymond

Wakati wimbo Unikumbushe wake Bahati pamoja na Ray Vanny wa WCB ukiendelea kufanya vizuri kwenye anga za vituo mbalimbali za televisheni na redio Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla, kuna vitu kadhaa vimejitokeza kwenye biwi la burudani.

Ubora wa video, mandhaari na maudhui ya ujumbe uliopo kwenye wimbo huu umeendana sambamba kabisa bila ya kupishana wala kukosana hivyo pongezi zinamrudia muongozi wa video hii mkenya X-Antonio.

Tukiachana na ubora wa video, kuna kipengele fulani kimejitokeza kwenye ukanda huu wa video wa wimbo huu mtamu na maridhawa. Kipande kidogo ambacho kinamuonesha Bahati akiwa kwenye mahojiano( Live interview) na mtangazaji wa televisheni. Lakini katika mukutadha huo, Bahati anajishaua na kujigamba mbele ya runinga na mwisho anainuka show ikiwa katikati na kung’tuka nje ya studio huku akimuacha mtangazaji akiwa hoi solemba hajui lipi la kufanya.

Je unamfahamu mtangazaji huyu? Anafahamika kama Larry Omondi Madowo. Ni kati ya watangazaji bora zaidi wenye wafuasi wengi zaidi nchini Kenya na pengine hapa barani Afrika. Yeye si mtangazaji wa habari tu kwenye runinga bali pia ni nguli katika uwanja wa habari zinazohusiana na teknolojia, matukio ya kisasa na burudani. Pia ni mwandishi katika gazeti la Kenya la ”Daily Nation” na ana kipengele chake pale kila siku ya Jumanne kinacho fahamika na wengi kama #FrontRow. Mbali na uandishi, Larry pia hutangaza kwenye kituo cha redio cha Nation FM kwenye kipindi chake kinachofahamika kama The Larry Madowo Show.

Kipindi cha burudani kinachorushwa kila siku ya Ijumaa kupitia runinga ya NTV nchini Kenya maarufu kama #The Trend, ndicho kimemfanya Larry kupendwa na kujikusanyia wafuasi lukuki nchini Kenya. Hata hivyo Larry mbali na NTV Kenya, ameshawahi kufanyia kazi vituo vya habari maarufu kama vile KTN Kenya na CNBC Africa.

Ni mtu anayependa kusafiri kwa sana katika nchi mbalimbali za dunia kila wiki, hivyo kupelekea watu ikiwemo mchekeshaji na staa wa comedy Adam & Eve Eric Omondi kumuuliza kama ana pasipoti ya kidiplomasia. Nimekusogezea moja kati ya (live interview ) ambayo Larry Madowo alikuwa amemkaribisha mchekeshaji Eric Omondi kwenye show yake ya #The Trend, Hebu burudika zaidi.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW