Fahamu

Mfahamu Mtanzania Profesa Handley Mwafwenga msomi mwenye digrii 7

Mfahamu Mtanzania Profesa Handley Mwafwenga msomi mwenye digrii 7

Akiwa na shahada tatu za uzamivu (PhD) na tatu nyingine za uzamili (masters), huenda Profesa Handley Mwafwenga ni miongoni mwa wasomi wenye shahada nyingi zaidi nchini hata duniani.

Tangu alipojiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuhitimu diploma ya juu ya kodi (advanced diploma) mwaka 1987, Profesa Mwafwenga hajawahi kuacha kusoma kiasi cha watu wake wa karibu kumshauri apumzike kidogo.Askofu (Alex) Malasusa na Waziri (Palamagamba) Kabudi walinishauri nipunguze kusoma.

Napenda kusoma kama wengine wapendavyo kusali, michezo au muziki,” anasema Profesa Mwafwenga ambaye hadi sasa ana digrii (shahada) saba tofauti za chuo kikuu na vyeti vingi vya kozi fupi alizosoma na kumpa mamlaka kitaaluma kuwa mchumi, mwanasaikolojia, mwanasheria na mshauri wa kodi.

Safari ya elimu ya Mwafwenga (52) ilianzia Shule ya Msingi Mwananyamala kabla hajajiunga Shule ya Sekondari Sangu na kumaliza kidato cha nne mwaka 1975.

Tangu akiwa mdogo, anasema baba yake.alikuwa anamwita profesa na wakati wote alimsisitiza kusoma kwa bidii.

Chanzo Mwananchi digital

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents