Burudani

Mfahamu mtayarishaji wa ‘African Beauty’ ya Diamond aliyomshirikisha Omarion, sio Lizer

By  | 

Ngoma bila mdundo (beat) ni sawa sawa na mboga bila chumvi. African Beauty ni mmoja kati ya ngoma ambayo inapatikana kwenye albamu mpya ya Diamond Platnumz, A Boy From Tandale. Mashabiki wamekuwa wakifurahia ngoma hiyo lakini wengi wao hawamfahamu mtayarishaji wake.

Producer Krizbeatz

Ngoma hiyo imetayarishwa na producer Chris Alvin Sunday maarufu ka jina la Krizbeatz kutoka nchini Nigeria.

Krizbeatz siyo jina geni kwa watu ambao wanafuatilia muziki wa Nigeria, tayari ameshawahi kutengeneza hits kibao kama ‘Pana’ na ‘Diana’ zote za Tekno, ‘Weekend Vibes’ ya Seyi Shay na nyingine.

Lakini pia mwezi Mei mwaka jana, Krizbeatz aliachia ngoma yake ‘Erima’ ambayo amemshirikisha Davido na Tekno.

Mwaka 2016 producer huyo alishika namba tatu katika orodha ya watayarishaji watano bora wa Nigeria kwenye Pulse Nigeria’s 2016.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments