Habari

Mfahamu Mwalimu ‘Maprosoo’ asubuhi darasani, jioni muuza mishikaki Mtwara ”Mke wangu akiniona nauza mishikaki nikimuita haji/ najenga nyumba kupitia ujasiriamali”

Josephat Mussa amekuwa mwalimu kwa miaka 16 na n afasi ya ualimu mkuu kwa miaka 11 kabla ya kushushwa daraja mwaka mmoja uliyopita kutokana na kutokuwa na kiwango stahiki cha elimu kwa ngazi hiyo.

 

Hali iliyopelekea kipato chake kuporomoka na kuamua kujiingiza kwenye ujasiriamali.

”Mke wangu na nafasi yake hakupenda kabisa, akiniona nauza mishikaki kituo cha basi hata nikimuita haji, baada ya saa za kazi ni mjasiriamali.” amesema mwalimu Josephat Mussa kwenye mahojiano yake na shirika la habari la BBC.

”Baada ya kuvuliwa tu madaraka, baada ya miezi mitatu na kuona maisha yamebadilika nikapata wazo la kuuza nyama, nikachoma mishikaki natembeza ili niweze kupunguza ukali wa maisha.”

”Lakini kubwa zaidi nacheza na ratiba yangu isije ikavuruga utataribu wa ajira yangu kwa sababu swala la ujasiriamali ni kazi ya ziada.”

”Idadi ya vipindi ninavyofundisha kwa wiki ni 18, naripoti kazini sa 12 na dakika 45 lakini baada ya hapo ratiba binafsi itaenedelea baada ya saa 9:30.”

”Ninafaida kubwa sana juu ya huu ujasiriamali, nina nyumba najenga nyingine kupitia kazi hii, mshahara unaoingia wala siugusi umetulia tu benk.”

Kwa miezi sita sasa mwalimu huyu maarufu kwa jina ‘maprosoo’ anachoma na kutembeza mishikaki katika mitaa mbali mbali ya mji wa Mtwara ili kumuwezesha kuendelea na ujenzi wa nyumba yake na kuipatia familia yake mahitaji bila ya kutegemea mshahara wake.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents