Fahamu

Mfahamu nabii Bushiri kiundani anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji pesa Afrika kusini

Nabii na mchungaji maarufu wa kikristo, raia wa Malawi al maarufu pastor Shepherd Bushiri, anakabiliwa na mashitaka 419 ikiwa ni pamoja na utakatishaji wa fedha nchini Afrika kusini.

Kutokana na mashitaka hayo mahakama ya Afrika Kusini ilitoa kibali cha kumkamata baada ya nabii huyokukwepa kutoa dhamani ya kumrejesha nchini mwake.

Mwishoni mwa juma Nabii Bushiri na mkewe Nabii Mary Bushiri, waliandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa waliondoka Malawi kwasababu ya masuala ya kiusalama mwaka 2015.

Prophet Shepherd Bushiri:

Mambo yalikuwa mabaya kwetu sote baada ya kukosa dhamana, alisema Nabii Bushiri.

Maafisa walimkamata yeye na mke wake mwezi Oktoba , 2020 na kumtuhumu kwa makosa ya wizi wa mamilioni ya dola na kuhusika katika sakata ya ufisadi.

Baadaye Novemba walimpatia yeye na mke wake dhamana ambayo ilikuwa na sharti kwamba lazima wasalimishe paspoti zao kwa mamlaka za Afrika Kusini.

Kuna hofu kuwa kesi hii inaweza kusababisha mzozo wa kidiplomasia kati ya Malawi na Afrika Kusini kwani watu wameanza kujiuliza maswali kuhusu hali za Bw Bushiri na mke wake na vipi waliweza kuingia nchini humo.

Bottles of oil wit Bushuri face ontop
“mafuta ya miujiza” nje ya kanisa

Shepherd Bushiri ni nani ?

Nabii Mchungaji Shepherd Bushiri ni mzaliwa wa Malawi ambaye huendesha shughuli zake za “unabii” katika makanisa mbalimbali kuanzia Ghana hadi Afrika Kusini.

Anadai kuwa anatibu virusi vya Ukimwi/HIV na kuwafufua watu, kwa mujibu wa magazeti ya Afrika Ksuini ya Mail & Guardian yaliyotolewa 2018.

Bushiri aliwahi kubashiri kuwa Uingereza itagawanyika, “majimbo” na itaingia vitani na kuwa katika “vurugu”, jarida la Maravi Post lilisema katika moja ya ripoti zake.

Na katika moja ya video zake alionekana akitembea hewani, video ambayo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii .

Bushiri alimwambia mwanasiasa wa Zimbabwe Kembo Mohadi kuwa atapata “madaraka ” hata kabla ya kutangazwa kuwa makamu wa rais, kulingana taarifa ya New Zimbabwe.

Pastor Shepherd Bushiri ni muanzilishi wa kanisa la Evangelical Church Gathering for South Africa lenye matawi yake katika nchi nyingine.

Wengi husema Mchungaji milionea ndiye kiongozi wa kidini tajiri zaidi barani Afrika.

Bushuri dey enta private jet
Anamiliki ndege zake binafsi

Anadai kuwatibu watu wenye virusi vya HIV, kuwafanya vipofu waone njia, anawabadilisha masikini kuwa matajiri, na hata wakati mmoja aliwahi kusema kuwa yeye anaweza kurejesha pumzi ya uhai ndaniya mtu aliyekufa.

Mchungaji Bushiri alikulia katika mji wa Mzuzu, uliopo Malawi kabla ya kwenda Pretoria nchini Afrika Kusini.

Taarifa zinasema kuwa alipigwa marufuku kukanyaga katika ardhi ya Botwana kwasababu ya “pesa za miujiza”.

Amekuwa maarufu sana kutokana na mikusanyiko mikubwa ya wafuasi wake wanaojaa katika viwanja vikubwa vya michezo.

Lakini watu wanamshutumu kuwa anawatumia vibaya masikini wanaotaka kubadili hali zao za maisha kwa kuwauzia “mafuta ya muujiza” .

Akifahamika kama Major 1 au Nabii Shepherd , Bushiri alizaliwa tarehe 20 Februari, 1983.

Mamlaka za Botwana zilifunga kanisa lake baada ya madai kuwa alikuwa anawataka watu wampatie pesa bila huduma yoyote, kitu ambacho kilikuwa ni kinyume na sheria za fedha nchini humo.

Prophet Shepherd Bushiri:

Mke wa Nabii Bushiri Mary ni nani?

Mary Bushiri ni mke wa Shepherd Bushiri. Anafahamika zaidi kama [Prophetess Mary Bushiri].

Alikuwa akifanya kazi kama muhasibu katika moja ya mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali . Lakini sasa amekuwa muhubiri sawa na mumewe.

Mary Bushiri na Shepherd Bushiri walioana Julai 2011.

Harusi ya Nabii Shepherd Bushiri ilifanyika katika uwanja wa michezo wa Mzuzu ,na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.

Prophet Shepherd Bushiri:

Kesi yake imefikia wapi?

Bushiri, na mke wake na watu wengine wawili wanakabiliwa na shutuma za kutakatisha fedha na mashitaka mengine 419.

Wapelelezi wa uhalifu wanasema kesi hiyo inahusu randza Afrika kusini milioni 102 ($6.6m).

Alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya Pretoria tarehe 21 Oktoba na kesi yake ilitarajiwa kuanza Mei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents