Michezo

Mfahamu refa wa mechi ya Chelsea na Man United Jumapili hii

Wikiendi hii katika ligi ya Uingereza kuna mechi kubwa mbili ambazo zinasubiriwa kwa hamu, je unazifahamu? Ni kati ya Chelsea dhidi ya Manchester United na nyingine ni Manchester City dhidi ya Arsenal.

Mechi hizi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili. Tuitazame mechi ya Chelsea dhidi ya United ambayo itachezwa katika uwanja wa Stamford Bridge, unamfahamu muamuzi ambaye amepangiwa kuchezesha mchezo huo? Basi tambua kuwa anaitwa Anthony Taylor na anaumri wa miaka 39.

Taylor amezaliwa katika eneo la Wythenshawe mjini Manchester na alianza kuchezesha mechi za ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka 2010 lakini kabla ya kufika hapo alianza kazi hiyo ya urefa tangu mwaka 2002 katika ngazi za chini.


Picha ya Anthony Taylor atakayechezesha mechi ya Chelsea na Manchester United Jumapili hii kjatika uwanja wa Stamford Bridge

Mwaka 2013 neema ilimuangukia Taylor kwa kuchaguliwa kuwa miongoni mwa waamuzi wa shirikisho la soka duniani Fifa. Huyu pia ndiye alichezesha mechi ya fainali ya kombe la FA msimu uliopita kati ya Chelsea na Arsenal katika uwanja wa Wembley ambapo Arsenal waliibuka washindi na kutwaa kombe hilo.

Refa huyu mpaka sasa ameshafanikiwa kuchezesha michezo 172 na ametoa kadi za njano 592 na kadi nyekundu 29.

Katika mchezo ambao atachezesha Jumapili hii, Taylor atasaidiana na waamuzi wengine Gary Beswick na Adam Nunn (wote washika vibendera) na Craig Pawson ambaye atakuwa kamisaa wa mchezo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents