Habari

Mfalme Akihito wa Japan ataka kung’atuka

Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung’atuka.

_90708160_4d9a31e3-2da1-4b7a-a5b3-dc56698c1516
Mfalme Akihito

Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.

_90708159_eeb9aef5-344e-49d7-9dd9-a3d3b3f8025f
Wananchi waonekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza matamanio yake ya kung’atuka

Kwa sasa, hakuna nafasi kisheria kumruhusu mfalme kuondoka madarakani Japan.

Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atathmini kwa makini matamanio ya mfalme huyo.

Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989.

Habari kwamba anataka kung’atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents