Tupo Nawe

Mfalme wa filamu Shah Rukh Khan, asherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa staili ya aina yake, Mashabiki wajazana nje ya nyumba yake – Video

Mfalme wa filamu Shah Rukh Khan, asherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa staili ya aina yake, Mashabiki wajazana nje ya nyumba yake - Video

Wikiendi hii iliyoisha ilikua ni siku ya kuzaliwa🎁🎂🍾 ya mfalme wa filamu Bollywood, Shah Rukh Khan🍹🕺🏼. Mkongwe huyo wa filamu ametimiza miaka 54.

Kumbukumbu yake ya kuzaliwa imesherehekewa na na idadi kubwa ya mashabiki nchini India ambao walijitokeza katika maeneo mbali mbali ili kuonyesha upendo kwa mwigizaji huyo.

Rafiki-aliyegeuka-adui-akageuka-rafiki-tena, Salman Khan alikuwa mmoja wa watu wa  kwanza kumtakia muigizaji huyo siku ya kuzaliwa kwake. Alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti video na timu yake ya Dabangg Tour ya Shah Rukh. Katika video hiyo, Salman pamoja na Jacqueline Fernandez, Daisy Shah, Maniesh Paul, Aayush Sharma, kaka Sohail Khan na Sonakshi Sinha ni miongoni mwa wengine waliweza kuonekana wakiimba wimbo wa siku ya kuzaliwa huku wakuiga saini yake.

https://www.instagram.com/iamsrk/

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW