Habari

Mfanyabiashara kizimbani kwa kukutwa na sare za jeshi

Casto Onyomolile Ngogo (35) mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es salaam, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la kukutwa na suruali 5,000 za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kwa Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba alidai kuwa Ngogo ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea,  alikutwa na vifaa hivyo katika maeneo ya bandari kavu ya Galco Inland Container (ICD) iliyopo Sokota Chang’ombe Juni 15 mwaka huu .

Wakili wa Serikali, Simon alidai kuwa siku hiyo, mshtakiwa huyo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ zenye thamani ya Shilingi 50 milioni ambazo zimepatikana kwa njia isiyo halali.

Juni 15 mwaka huu, Ngogo anadaiwa kuwa katika eneo hilo alikutwa na maofisa wa Jeshi la Polisi akiwa na tisheti 50 za JWTZ zenye thamani ya Shilingi 500, 000.

Hata hivyo mshtakiwa  hakuruhusiwa kusema chochote kwa sababu shtaka lake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents