Habari

Mfumo wa tiketi za kielekroniki kufungwa uwanja wa taifa Dar

Waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo, Nape Nnauye, amesema mfumo wa tiketi za kielektroniki utasaidia kuboresha mapato kwenye uwanja wa taifa na pia utaondoa usumbufu kwa mashabiki wa mpira.

napelaana-620x400

Nape ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika uwanja wa taifa kwa lengo la kujifunza mafunzo maalumu ya matumizi ya tiketi za kielektroniki ambao tayari mfumo huo umeshafungwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

“Ninajua mfumo huu kwasababu utaharibu ulaji wa watu utakuwa na vita kubwa , mimi nimetaka nyie mniunge mkono kwenye vita hiyo tushinde, tukishinda itasaidia sana, itasidia michezo yetu, itasaidia mapato ya serikali,lakini itasaidia na hao wanaovuja jasho lao wapate haki yao,”,alisema Nape.

“KwasabaBu katika hali ya kawaida mnakusanya milioni 700 mnaambiwa milioni mia 200 mia 300 maana yake kuna watu wamevuja jasho lao hawatapata haki yao,”aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents