Habari

Mganga Mfawidhi asimamishwa kazi kwa kukiuka maagizo ya serikali

Baada ya serikali kupitia Wizara ya Afya, Jinsia ,Wazee na Watoto, kupiga marufuku mama mjamzito, mtoto chini ya miaka mitano na mzee kutotoa pesa ya matibabu. Waziri Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi, Dkt. Mpola Tamambele kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo hayo.

Kusimamishwa kazi kwa Mfawidhi huyo kuna kuja baada ya mama aliyejifungua, Bi Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma .

Waziri huyo mwenye dhamana hiyo, kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea .

Waziri Ummy aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi ,kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo ,Hamoud Jumaa.

“Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho ,“ alisema Waziri Ummy.

“Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika .”

Na Emmy Mwaipopo

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents