Mgao umeanza tena

Mgao umeanza tena
Tanesco limeanzisha mgawo wa dharura wa umeme kwa jiji la Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana na pia kuanzia saa 12 jioni hadi nne usiku, kutokana na kukosa huduma ya mitambo miwili ya kuzalisha umeme ya kampuni ya Songas.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Tanesco jana iieleza kuwa mtambo mmoja uko katika matengezo yaliyopangwa kiufundi na mwingine umeharibika na hivyo kusababisha umeme unaosambazwa jijini kupungua kwa megawati 53.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Tanesco, matumizi ya umeme katika miji ya Dar es Salaam na Zanzibar ni megawati 355 na upungufu wa umeme unaofuliwa na mitambo hiyo ya Songas isababisha kuongezeka kwa umeme unaopita kwenye transfoma zinazopeleka umeme kwenye miji hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Tanesco inaeleza kuwa kiufundi kunasababisha transfoma mbili zilizopo kitua cha umeme cha ubungo kuelemewa kuliko ilivyo uwezo wake.

Tanesco katika taarifa yake hiyo imesema iko katika mchakato wa kununua transfoma nyingine na kuiweka Ubungo ili kuzuia tatizo kama hilo lisitokee tena hapo baadaye.

"Kutochukua hatua ya kufanya mgawo, kutasababisha kukatika kwa umeme kwenye gridi nzima ya taifa katika majira ya asubuhi na jioni, kutokana na kuzidiwa kwa transfoma za Ubungo," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano, Tanesco, makao makuu.

Mgawo huo umekuja wakati ambapo umma wa Watanzania tayari umetangaziwa kuhusu uwezekano wa nchi kuingia gizani, kutokana na serikali kutonunua jenereta za kampuni ya Dowans.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents