Habari

Mgogoro wa jina la kundi kongwe la R&B ‘Blackstreet’ waibuka

Wakati makundi mengine yaliyopotea likiwemo Backstreet Boys yakiungana tena kupanga kufanya ujio mpya, kundi kongwe la R&B la miaka ya 90 BLACKSTREET lina ugomvi wa umiliki wa jina la kundi hilo.

Blackstreet

Mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo aitwaye Chauncey Black ameonekana kutoridhishwa na jinsi member mwenzie Teddy Riley anavyofanya baadhi ya mambo katika kundi.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Black anadai kuwa yeye ndie mmiliki wa sasa wa jina “Blackstreet” na Teddy amekuwa akilitumia kinyume na bila idhini yake. Kwa hali ya kushangaza kwa members wa kundi moja kugombania umiliki wa jina la kundi, Black aliendelea kusema kuwa originally Teddy ndie aliyekuwa mmiliki wa jina hilo hapo awali lakini umiliki wake uli expire na hivyo yeye ndio akalichukuwa na kuwa mmiliki mpya.

Kwa mujibu wa Black, Riley amekiuka haki za umiliki wa jina la kundi hilo kwa kuperform na bendi nyingine na kutumia jina la Blackstreet, na alipoulizwa kwanini haperform na wenzake tena kama kundi alisema hawezi tena kuperform na Riley sababu haonyeshi ushirikiano.

Kwa upande wa Riley, mwakilishi wake ameuambia mtandao huo kuwa wao kwa sasa hawana cha kuzungumza kuhusiana na madai ya kijinga yaliyotolewa na Chauncey Andre Hannibal aka’Black .

Kundi la Blackstreet lilianzishwa mwaka 1991 na mpaka sasa bado liko hai na members wake akiwemo Teddy Riley ambaye ndio kiongozi wa kundi, Dave Hollister, ‘previous touring member’ Sherman “J-Stylz” Tinsdale, Lenny Harold na Tony Tyler, lakini Black hayuko tena kwenye kundi hili.

Jikumbushe kwa kutazama moja ya hit songs zao za miaka ya 90, No “Diggity” waliowashirikisha Dr. Dre na Queen Pen

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents