Afya

Mgonjwa agunduliwa na meno bandia yaliokwama kwenye koo lake baada ya kufanyiwa upasuaji

Mgonjwa agunduliwa na meno bandia yaliokwama kwenye koo lake baada ya kufanyiwa upasuaji

Mgonjwa mmoja amepatikana meno bandia yaliokwama kwenye koo lake siku nane baada ya kufanyiwa upasuaji wa tumbo. Mtu huyo wa miaka 72 alilalamika kuwa na tatizo la kumeza chochote na kwamba anakohoa damu kabla ya madaktari kugundua amemeza meno bandia. Alirudi hospitali mara kadhaa, kufanyiwa upasuaji mwingine na hata kuongezewa damu ili kurekebisha hitilafu hiyo ya kimatibabu.

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Paget mjini Norfolk, nchini Uingereza wamesema kuwa wamefanyia marekebisho utaratibu wa kumkagua mgonjwa kabla ya kufanyiwa upasuaji. Kisa cha mwanamume huyo kimechapishwa katika ripoti ya jarida la BMJ, ambayo waandishi wake wamependekeza mgonjwa atolewe meno bandia kabla ya kudungwa sindano ya kufisha ganzi mwili mzima. Siku sita baada ya kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe tumboni mwake, mtu huyo alirudi katika hospitali hiyo kuwafahamisha madaktari alikuwa na tatizo la kumeza chakula.

Picha ya Xray ya kooHaki miliki ya pichaBMJ CASE REPORTS 2019
Image caption
Kwa mujibu wa BBC. Picha ya Xray ya koo inaonesha meno hayo bandia yakiwa yamekwama kooni na kumzuia muathiriwa kula, kupumua na kulala

Madaktari katika hospitali ya Gorleston nchini Uingereza wanaamini ilikuwa maabukizi ya mfumo wa kupumua kutokana na athari ya kuwekewa mipira kooni wakati wa kufanyiwa upasuaji, na kumuandikia dawa aina ya antibaiotiki na steroids. Lakini mwanamume huyo aliporudi tena siku mbili baadae, wahudumu wa afya walichunguza koo yake na mfumo wa kutoa sauti- na ni hapo walipogungua kuna kitu chenye muundo wa duara nusu ambacho kimeziba sehemu ya koo lake. Baadae aliwaambia amepoteza meno yake bandia – meno matatu na sehemu ya juu ya ndani ya mdomo – wakati alipokuwa amelazwa hospitali hapo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji. Baada ya upasuaji mwingine wa kuondoa meno hayo bandia aliruhusiwa kwenda nyumbani alkini alirudi tena mara nne hospitali akiwa na tatizo la kutokwa na damu. Wakati wataalamu walipogundua damu hiyo inatoka kuuni mwake alikuwa amepoteza damu nyingi kiasa cha kuhitaji kuongezewa damu.

Hospitali ya chuo Kikuu cha James Paget
Image captionHospitali ya chuo Kikuu cha James Paget

Mtayarishi wa ripoti hiyo amesema visa vingine kama hivyo vimewahi kushuhudiwa ambapo watu wamewahi kumeza meno bandia baada ya kudungwa sindano ya kufisha ganzi. Kawaida mgonjwa huulizwa kama ana kiungo chochote bandia kama meno mwilini mwake na meno hayo hutolewa kabla ya mgonjwa kufanyiwa upasuaji, waliongeza. Mkurugunzi wa Hazel Stuart, katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget, amesema hatua hiyo ilikuwa imefanywa. “Kutokana na kisa hiki, mchakato huo umechunguzwa upya, na kufanyiwa marekebisho, na wafanyikazi kuhusishwa vilivyo katika utaratibu huo,” alisema.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents