Michezo

Mgosi kurudia ya Messi

Ikiwa imebaki siku moja kabla ya mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga washambuliaji mahiri wa timu hizo wameanza majingambo. Mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amewataka mashabiki wa Yanga kujiandaa na kile alichokifanya Lionel Messi wa Barcelona kwa Arsenal katikati ya wiki hii.

Mgosi ambaye ameshafunga mabao 14 kati ya 42 yaliyofungwa na Simba msimu huu, ameahadi kufanya mauji makubwa dhidi ya Yanga kama alivyofanya Messi kwa kufunga mabao manne dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania, Mgosi ambaye hadi sasa ameshafunga jumla mabao 16 katika mechi 22 za michuano yote ya kimataifa akiwa Simba msimu huu.

Nyota huyo anawastani wa kufunga bao moja kwa mechi za ligi na Kombe la Shirikisho Afrika, pia anaingia kwenye mchezo huo akiwa na kumbukumbu kwamba yeye ndiye aliyekuwa mfugaji wa bao pekee dhidi ya Yanga mwezi Oktoba mwaka jana.

Mgosi alisema kuwa amepania kuwapa raha mashabiki wao kwa kuwafungia mabao 4, katika mchezo wao dhidi ya Yanga, hapo Jumapili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Alisema lengo lake ni kuibuka mfungaji bora anajuwa kwa msahada wa wachezaji wenzake atafanisha lengo ilo na kuisaidia Simba kutegeneza historia mpya msimu huu.

“Nia ni kuakikisha katika msimu huu hawafungwi na mechi hata moja hivyo itakuwa ni ngumu sana historia yao kualibiwa na Yanga wakati raundi ya kwanza waliwafunga bao 1-0.”

Hata hivyo; mpinzani wake kwenye mbio za ufungaji bora Mrisho Ngassa anayesaka rekodi ya kuifunga Simba kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye mchezo huo uliojaa malengo ya kuvunjwa kwa rekodi ya pande zote.

Alisema mechi hiyo ni kama fainali kwake na Mgosi kwani kila mmoja atataka kuchukua kiatu cha dhahabu kwa msimu huu kwani atakayepoteza hapo ndio atakuwa amekosa kiatu hicho.

Ngassa aliongeza kuwa mechi hiyo wao wanaiona kawaida baada ya kugundua udhaifu wa Simba walipocheza nao kwenye michuano ya Kombe la Tusker ambako Yanga ilipata ushindi katika mchezo wa bao la dakika ya 118 lilofungwa na Shamte Ally.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents