Habari

Mh. Lissu anena mazito juu ya wanaohama CHADEMA

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye alipigwa risasi Septemba 7 mwaka huu amesema kuwa suala la viongozi wa wanasaliti CHADEMA lisiwatishe bali wao waendelee na kazi yao huku akisema kuwa sio ajabu hata kidogo kwani hata Yesu aliwahi kusalitiwa na mwanafunzi wake.

Tundu Lissu ameyaeleza hayo alipokuwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Taifa, Patrick Ole Sosopi ambaye alimtembelea Mhe Lissu hospitali jijini Nairobi jana kumjulia hali. Ambapo Sosopi ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza hivi:

KUTOKA NAIROBI HOSPITAL

Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipatia kibali cha kufika Nairobi Hospital kumtembelea na kumjulia hali Mhe. Tundu Antipas Lisu, aliyelazwa kwa takribani miezi mitatu sasa kwa shambulio la kinyama lililofanywa na watu wasio julikana ndani ya kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano.
Ndugu zangu nimepata faraja na furaha kubwa ya kumuona Kaka yangu, Rafiki yangu na Kiongozi wangu Tundu Lisu akiwa katika hali nzuri sana na mwenye ujasiri mkubwa asiye kata tamaa.
Nilitegemea zaidi mimi kumtia moyo na faraja lakini yeye ameweza kunitia moyo zaidi.
Lisu anasema hii ndiyo gharama wanayopaswa kuipata wapambanaji wote hata historia inaonyesha au kutukumbusha. Amepigwa risasi kwa sababu ya misimamo yake katika kupigania haki, ameapa kukabiliana na gharama hii na yoyote atakayo ipata ili kuwaletea haki Watanzania.

Ndugu zangu Mhe Lisu ameweza kunieleza mambo mengi sana na binafsi naamini ameniagiza kwa niaba ya Baraza la Vijana na tutayetekeleza kwa maslahi mapana ya nchi na chama chetu.
Mhe. Lisu hajasita kuniambia kwamba hali ya siasa yetu ndani ya nchi yetu kwa Biashara inayoendelea kununua Viongozi uchwara na wenye tamaa wa chama chetu, amesema tusipate hofu CHADEMA hatujaanza kusalitiwa leo na hao wanaondoka, sio ajabu hata kidogo kwani mbona Yesu aliwahi kusalitiwa tena na mwanafunzi wake na hakuacha kazi yake…wanaotusaliti hawajawahi kuwa na mafanikio katika maisha yao, tusikate tamaa mapambano yaendelee… Mwisho kabisa Mhe. Lisu ametuma salamu nyingi kwa Watanzania wote wanaoendelea Kumchangia na Kumuombea, ameendelea kuwasihi waendelee kumchangia na kumuombea, maana Bunge na serikali wamekataa kabisa kumtibia kwa mujibu wa sheria na ni haki yake.
Ndugu zangu, naomba kuwahikishieni Mhe. Tundu Lisu atarudi kwa mapambano tena sisi tuendelee atakapokuja kutukuta naye ataungana nasi.
…aluta continua…
Get Well Soon Mhe. Tundu Lsu

Patrick Ole Sosopi
Mwenyekiti BAVICHA Taifa..
Nairobi-Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents