Habari

Mh Lissu hajashambuliwa na majambazi – Godbless Lema

Wakati Tundu Lissu akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini kenya, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita, bado hakuna taarifa rasmi ambayo inaeleza ni nani amefanya tukio hilo la kinyama.

Jumatano hii Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kwa kudai kuwa tukio la Lissu kushambiliwa lilipangwa na kikundi cha watu na sio majambazi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Suala la Mh Tundu Lissu ni organized, ni mpango ambao umepangwa, Mh Lissu hajashambuliwa na majambazi, Mh Lissu alianza kusema anafuatiliwa siku nyingi na hata ukiangalia hilo jaribio la mauwaji yale lilivyotaka kufanyika unaona kabisa ni jambo lilipangwa vizuri kabisa, Mh Lissu ni mtu wa watu na wakati mwingine tunafanya vikao mpaka saa nane usiku kwahiyo kama shambulio la Mh Lissu lilikuwa lina lengo la kihalifu watu wangeweza kumsubiri akitoka Dar es salaam kuja Dodoma usiku, wangemsubiri jimboni kwake usiku lakini jambo hili limefanywa kutisha wazungumzaji wengine kama sisi, jambo hili ni lengo la kupeleka meseji kwamba tunaweza tufanya kitu chochote na msitufanye kitu chochote na unafahamu,” Lema aliiambia BBC.

Kwa upande wa afya yake, Mchungaji Peter Msigwa-mbunge Iringa mjini alisema bado afya ya mwanasiasa huyo haijaweza kukaa vizuri kwani bado upo kwenye wodi ya watu wenye ungalizi maalumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents