Habari

Mh. Nyalandu atinga rasmi Chadema

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Aikael Mbowe amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho, Lazaro Nyalandu aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM na kujiondoa Uanachana Oktoba 30 mwaka huu.

Mh. Nyalandu amekabidhiwa kadi hiyo Jumapili hii katika uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu ambako Mbowe alikuwa anahutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26,2017.

“Ndugu zangu wananchama wa Chama changu kipya pendwa Chadema wananchi wote mliohudhuria hapa, nitumie neno ninalo lipenda sana amani iwe nanyi, na simama mbele yenu leo na simama mbele ya Watanzania nikiwa nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya kujiunga na harakati za kupigania mageuzi ya kisiasa, mageuzi ya kijamii, mageuzi ya kiuchumi nchini kwetu Tanzania,” alisema Nyalandu.

Hata hivyo Nyalandu alisema kuwa katika miaka miwili ya uongozi wa Awamu ta Tano ameaminia na kujiridhisha kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kimepoteza mwelekeo wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents