Habari

Mh. Zitto anena baada ya gazeti la MAWIO kufungiwa

Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT-Wazalendo), Zitto kabwe amepinga vikali hatua ya kufungiwa kwa gazeti la MAWIO na kudai kuwa hatua hiyo inawanyima wananchi mawazo mbadala.

Mh. Zitto ameyasema kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo amesema uamuzi wa kulifungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila Mwanademokrasia.

Uamuzi wa kufungia gazeti la Mawio unapaswa kulaaniwa na kila mwanademokrasia. Uhusika wa Marais wastaafu kwenye mikataba ya madini umesemwa na Rais Magufuli Mwenyewe sio Mawio. Hakuna mkataba ulioingiwa bila Baraza la Mawaziri kuidhinisha. Kitendo cha Kamati ya Rais kutuhumu Mawaziri wa zamani mbele ya Rais Magufuli na yeye Mwenyewe Rais Magufuli kusema hatapona mtu ilikuwa ni dhahiri kuwa Rais anawachimba watangulizi wake.
Kwa sisi tuliofundishwa lugha ya Uongozi tuling’amua mapema kuwa Rais Magufuli alikuwa anawatuhumu wenzake. Hivyo Gazeti la Mawio lilitafsiri tu maelezo ya Rais.
Kitendo cha Rais kuonya kuwa Marais wastaafu waachwe ilikuwa ni KUJISEMESHA tu na kufungia gazeti la Mawio ni ‘ panick ‘ ya Rais Magufuli baada ya kuwasema watangulizi wake. Kila wakati Rais analia kuhujumiwa na kutaka kuombewa; Adui wa Magufuli ni Magufuli mwenyewe.
Serikali ifungulie Gazeti la Mawio mara moja bila masharti kwani kulifungia ni kuwanyima Watanzania mawazo mbadala kuhusu mambo ya hovyo yanayoendelea nchini kwetu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents