Habari

Mh. Zitto hatarini

Kuna habari kuwa Mbunge machachari wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe yuko katika hatari kubwa baada ya kutishiwa kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wapinzani wake kisiasa.

Na Usu-Emma Sindila, Jijini



Kuna habari kuwa Mbunge machachari wa Kigoma Kaskazini, Mhe. Zitto Kabwe yuko katika hatari kubwa baada ya kutishiwa kuuawa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wapinzani wake kisiasa.


Habari toka kwa watu walio karibu na Zitto, zinadai kuwa vitisho anavyodaiwa kuvipata mbunge huyo toka kwa wapinzani wake, vinadaiwa kutumwa kwa njia ya meseji za simu.


Watu hao wa karibu ambao hawakupenda kuandikwa majina yao, wamesema watishaji wa maisha ya Zitto wanadaiwa kumueleza kuwa asipokuwa makini na kuendelea `kuchonga` juu ya suala la mikataba ya madini ambalo ni kubwa kuliko uwezo wake, basi ajiandae kwenda kuzimu.


Imedaiwa kuwa mbunge huyo amesisitizwa kuwa awe mpole kuhusiana na mambo hayo kwa kuwa yeye hajui chochote kuhusiana na nchi inakoelekea.


Alipoulizwa juu ya madai hayo katika mkutano na waandihi wa habari jana pale kwenye Makao Makuu ya chama chake cha CHADEMA, Mhe. Zitto alisema hilo ni suala la kipolisi na hivyo yeye hawezi kulizungumza.


Aidha, aliwataka waandishi wa habari waliokuwa wakitaka kujua undani wa madai hayo ya vitisho, kuwawasiliana na Mkurugenzi wa Kamati ya Ulinzi ya CHADEMA, akidai kuwa yeye ndiye anayefahamu zaidi kuhusiana na suala hilo.


Hata hivyo, alipofuatwa baadaye na mwandishi wa Alasiri, Zitto akasisitiza kuwa yeye hawezi kulisema.


`Jamani si kila kitu cha kuweka hadharani hukawii kusema ni kweli, halafu kesho ukakuta liko front page (kurasa za mbele) ya magazeti yote nchini,` akasema.


Hata polisi walipoulizwa leo asubuhi na gazeti hili iwapo wamepokea taarifa zozote kutoka kwa Bw. Zitto kuhusiana na vitisho hivyo, walisema hawajapokea taarifa hizo.


Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents