Habari

Mh. Zitto Kabwe amjibu Polepole

Baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole kumtuhumu Mhe. Zitto Kabwe kupotosha taarifa za CAG kuhusu kupotea kwa shilingi trilioni 1.5, kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo ameibuka na kujibu mapigo.

Zitto ametumia mtandao wa Twitter kujibu tuhuma hizo za Polepole kwa kumwambia amekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka nane hivyo anafahamu kile anachokisema.

“Serikali ya CCM ilidhani Watanzania ni mandondocha,wanapelekwa pelekwa tu. Nimekuwa Mwenyekiti wa PAC/POAC kwa miaka 8. Ninajua ninachosema.” ameandika Zitto.

“Jumla ya TZS trilioni 1.5 hazina maelezo ya matumizi yake Katika mwaka 2016/17. Sitajibishana na Mwenezi wa CCM, yeye size yake @AdoShaibu,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents