Habari

Mh. Zitto kufanya ziara Kata zinazoongozwa na ACT Wazalendo

Chama cha ACT- Wazalendo kupitia Kiongozi wake, Zitto Kabwe pamoja na viongozi wengine wa chama hicho wameanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Zitto kupitia taarifa yake aliyoitoa leo, imeeleza kuwa lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi na kushiriki kazi za maendeleo katika Kata hizo.

Leo, nikiwa pamoja Na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Serikali za Mitaa, Mama Annamarrystella Mallack, Katibu wa Kamati hiyo, ndugu Janeth Joel Rithe, pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Sera na Utafiti, ndugu Emmanuel Mvula tumeanza ziara ya mikoa 8 kutembelea Kata mbalimbali ambazo wananchi walichagua Madiwani kutoka chama chetu cha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Lengo la ziara ni kuwashukuru wananchi, kushiriki kazi za maendeleo katika kata, kuzungumza na kamati ya maendeleo ya kata, kuzungumza na wananchi wa kata husika, kuangalia utendaji wa madiwani kutokana na matarajio ya wananchi, kuona vikwazo na changamoto za Madiwani wetu, kusisitiza Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa wananchi kwenye masuala yote ya Kata, pamoja na kufanya tafiti juu ya masuala ya kisera pamoja na miradi ya maendeleo ambayo ACT Wazalendo Taifa tunaweza kuyabeba kusaidia madiwani wetu.

Ziara itafanyika kwa siku 19 katika mikoa 8 husika, ambako leo tumeanzia Kata ya Kiparang’anda, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Kiparang’anda
Mkuranga
Pwani
Februari 19, 2018

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents