Uncategorized

Mhadhiri wa saikolojia na sayansi ya ubongo ataja njia tano za kujitengenezea furaha, ikiwa leo dunia huadhimisha siku hiyo

Kila ifikapo tarehe 20 ya mwezi Machi dunia huazimisha siku ya furaha, licha ya miongoni mwa watu wengi kukosa hiyo furaha yenyewe na hii ni njia ya kuirejesha.

Kama wanavyvojifunza wanamuziki na wanariadha kuwa bora na kufanikiwa, basi inabidi na wewe ufanye vivyo hivyo iwapo unataka kuwa na furaha.

Kwa mujibu wa shirika la BBC, Mhadhiri wa saikolojia na sayansi ya ubongo kutoka chuo kikuu cha Yale nchini Marekani, Laurie Santos amesema “Huwezi tu kuwa na furaha, ni lazima ujizoezeshe wanasema wataalamu,”

Image result for laurie santos

Mhadhiri wa saikolojia na sayansi ya ubongo kutoka chuo kikuu cha Yale nchini Marekani, Laurie Santos

Na Santos yupo katika nafasi nzuri ya kutuonyesha namna ya kuepukana na huzuni: darasa lake “Saikolojia na maisha mazuri ” lina umaarufu mkubwa katika historia ya miaka 317 ya chuo hicho kikuu cha Yale.

“Sayansi imedhihirisha kwamba kuwa na furaha inahitaji jitihada za makusudi. Sio rahisi na huchukua muda”, anasema Santos, lakini linawezekana.

Na hivi ndivyo unavyoweza kufanya hivyo kwa mujibu wa vidokezo vitano vikuu vya Professor Santos kukusaidia kuipata furaha maishani mwako:

1. Tengeneza orodha ya kuwa na shukrani/ kuwa na tabia ya kushukuru

A smiling, young, bearded man in eyeglasses and yellow shirt holding hands up in feeling of happiness and gratitude - blue background.

Santos amewataka wanafunzi waandike mambo ambayo wanashukuru kuwa nayo maishani mwao – kila siku usiku kabla, kwa muda wa wiki nzima.

Hii inakuwa orodha yao ya mambo wanayoshukuru kuwa nayo.

“Huenda likaonekana kuwa jambo rahisi lakini tumewaona wanafunzi wanaofanya zoezi hili kila siku na wanaonekana kuwa na furaha zaidi”, anasema Santos.

2. Lala zaidi na kwa muda mrefu

Young woman in a blue coat sleeping on a meadow

Changamoto ni kujitahidi kulala kwa saa nane, kila siku kwa wiki nzima.

Huu umeonekana kuwa mtihani mkubwa zaidi kuutimiza kwa mujibu wa Santos.

“Huenda likaonekana kuwa jambo la ujinga, lakini tunajua kwamba kulala kwa muda zaidi na usingizi mzuri kunapunguza nafasi ya wewe kuugua msongo wa mawazo na huimarisha tabia ya mtu ,” amesema Santos.

3. Tafakari

Young woman meditating on a sofa at home, plants on the background and a big, light, window to her left

Chukua muda wa dakika angalau 10 kila siku kukaa na kutafakari kila siku.

Santos anasema alipokuwa mwanafunzi ilimsaidia sana kufanya hivyo.

Sasa yeye ni mhadhiri anawaeleza wanafunzi wake kwa kutumia tafiti mbali mbali zinazothibitisha kwamba kutafakari na mazoezi mengine yanayochangamsha akili yanaweza kukusaidia kuwa na furaha zaidi.

4. Jiliwaze na uzungumze na familia na rafiki

A father and a child, camping, admiring the starry night sky

Kwa mujibu wa Santos, kuna utafiti unaoongezeka unaobaini kwamba kuwa na muda mzuri na muafaka na familia na marafiki wa karibu inasaidia kupata furaha.

Kukaa na watu tunaowapenda – au kuwa na mahusiano ya karibu katika jamii – kimtazamo wa kisaikolojia – insaidia kuimarisha afya yako.

Sio jambo kubwa, anasema Santos, hakikisha tu “unajivinjari, utambue kwamba umetenga muda huu kuwa na walio karibu na wewe, na utambue namna munavyotumia muda huo”.

5. Punguza uhusiano wa katika mitandao ya kijamii na idhinisha mahusiano halisi

A couple jumping into beautiful blue water

Huenda tukapata furaha isiyo halisi kutoka marafiki wa mitandao ya kijamii anasema Santos, na anasema ni muhimu mu asijisahau na hilo.

“Utafiti wa sasa unaonyesha watu wanaotumia mitandao ya kijamii kama Instagram , huwa hawana furaha ikilinganishwa na wasio tumia mitanao hiyo sana.”

Ndio hayo basi:

iwapo unataka kuwana furaha ya dhati maishani, anza kwa kuwa mtu mwenye shukrani zaidi, lala unono usiku, jipunguzie mawazo, na jiliwaze na watu wanaokupa furaha na unaowapenda na achana na mitandao ya kijamii kwa kiasi fulani.Iwapo kwa wengine linawasaidia, na wewe vile vile linaweza kukusaidia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents