DStv Inogilee!

Mhe. Mbowe na Esther Matiko washinda rufaa dhidi ya DPP, warudishwa mahabusu

Mahakama ya Rufaa imetupilia mbali rufani ya DPP ya kupinga Mahakama Kuu kusikiliza rufani ya kupinga Freeman Mbowe na Esther Matiko kufutiwa dhamana.

Mhe. Mbowe na Matiko
Mahakama ya Rufaa imeagiza jalada la kesi lirejeshwe Mahakama Kuu kwa ajili ya kuendelea kusikiliza maombi ya washtakiwa ya kutenguliwa dhamana yao.
Jopo la majaji limesema rufaa ya DPP haina mashiko na kwamba Jaji Sam Rumanyika alikuwa sahihi kukubali kusikiliza rufani ya kupinga kutenguliwa dhamana ya washtakiwa.
Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri mnamon Novemba 23 mwaka 2018. Baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW