Habari

Mhe. Nape afunguka sababu za kuhoji vitu vingi mitandaoni baada ya kutumbuliwa (+Video)

By  | 

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa mitandao ya kijamii na umemfuata, Mbunge wa Mtama, Mhe. Nape Nnauye bila shaka utaona vitu vingi akihoji kutokana na hali ya siasa ilivyo nchini.

Mhe. Nape Nnauye

Sasa ukweli  ni kwamba vitu ambavyo anaandika ni maoni yake kutoka moyoni kwani amesema kipindi akiwa Waziri wa Habari, na hata alivyokuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi alikuwa yupo kwenye serikali na alikuwa na uwezo wa kukutana na Mawaziri wakazungumza na mambo yakaenda sawa, tofauti na sasa ambapo akiona jambo limekosewa sehemu pekee ya kuliongelea au kushauri ni kupitia kwenye Mitandao ya kijamii, Bunge na mikutano ya hadhara.

kuna watu wanaanza kumchambua Nape kuanzia alipokuwa Waziri nadhani ukianzia hapo utakuwa unakosea..Mimi nimeingia kwenye ujumbe wa Halmashauri kuu kuanzia mwaka 2002, miaka 15 iliyopita na nadhani ni moja ya watu ambao nilikuwa naongea sana, Mimi ni mtu ambae na speak on my mind… Nakumbuka kipindi kile sisi ndiyo tuliibua dhana ya wabunge mizigo, serikalini,“amesema Nape Nnauye huku akieleza sababu za kuandika maoni yake mitandaoni

Unapokuwa Waziri unakuwa sehemu ya serikali na unakuwa na room ya kwenda kwenye baraza la mawaziri sasa ukiwa na room ya kumshauri Rais halafu unaenda barabarani watu watakushangaa… huenda haya ninayoyafanya nilikuwa nafanya nilipokuwa Waziri,“amesema Mhe. Nape Nnauye, Tazama mahojiano yake yote hapa chini akifunguka zaidi

 

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments